NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, May 3, 2010

RAIS KIKWETE ANAFANYA VIZURI ANAPOFANYA HIVI

 • Picha hizi za Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete zinahuzunisha, zinafariji na pia zinatia matumaini. Zinahuzunisha kwa sababu zilipigwa wakati Rais alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Evaristi Semeni - mtoto mwenye umri wa miaka kumi na moja aliyefariki katika ajali ya kugongwa na gari tarehe 26/4/2010 jioni katika kijiji cha Msoga ambapo yeye pamoja na watoto wengine wawili walifariki dunia.
 • Unaweza kuiona huzuni katika uso wa raisi pamoja na baba mzazi wa Marehemu Evaristi Semeni. Tulikuwa tumezoea kuwaona viongozi wa ngazi za juu wakihudhuria mazishi ya familia zenye majina. Picha hii inagusa hisia sana na inamwonyesha raisi katika ubidanamu na utu wake kabisa. Naamini kwamba mzazi huyu, pamoja na huzuni yake yote ya kuondokewa na mtoto wake, alifarijika kwa pole na faraja iliyoletwa na ujio wa kiongozi mkuu wa nchi.
 • Hapa Rais yupo na waombolezaji ndani ya nyumba. Na ukitazama vizuri utaona. Haya ndiyo maisha halisi ya Watanzania wa vijijini ambao kwa bahati mbaya ndiyo wengi. Sijui Rais anawaza nini...
 • Hapa Rais anatoka nje kwenda kuungana na waombolezaji wengine. Nimefikiri mambo mengi sana baada ya kuzitazama picha hizi. Pengine safari kama hizi za viongozi wa kitaifa kwenda kuyaona maisha halisi ya Mtanzania wa kawaida kule kijijini zinaweza kuwa kichocheo kinachoweza kuiamsha upya ari mpya na kuhakikisha kwamba kweli maisha bora kwa kila Mtanzania yanapatikana tena kwa kasi mpya na nguvu mpya!
 • Mungu Awalaze marehemu mahali pema peponi; na tunamuunga mkono rais kwa kwenda kuungana na wananchi hawa wa kijijini katika huzuni yao; na kama alivyosema Mjengwa, kuwapelekea mwanga katika giza lao na matumaini katika hali yao ya kukata tamaa.

3 comments:

 1. Dah! Hizi picha zimenifanya nitoke machozi. Hivi hawa mafisadi wanafikiria nini wanapoona Watanzania wenzao wanaowaibia wanaishi katika hali kama hii? Rais Kikwete is a decent, intelligent and dedicated working man lakini mafisadi weshamzidi kete. Si haki kuona kuwa natural resources zetu zinakuwa taken na hawa mafisadi wachache wakati wananchi wetu wanaishi katika hali kama hizi. Mafisadi, rudisheni hayo mabilioni yaende yakasaidie Watanzania wenzenu.

  Kama mimi ningekuwa Rais ningewaamuru mafisadi wote waende wakakae wiki moja katika hiyo nyumba ili waone how it feels.

  Kiwete - we are behind you on this. Safisha serikali yako na asante kwa kuwajali wananchi wako hasa hawa masikini who have nothing. It means a lot to us as human beings and as Tanzanians. May God bless our beautiful Tanzania inayotafunwa na wajanja wachache!

  ReplyDelete
 2. Dah! Hizi picha zimenifanya nitoke machozi. Hivi hawa mafisadi wanafikiria nini wanapoona Watanzania wenzao wanaowaibia wanaishi katika hali kama hii? Rais Kikwete is a decent, intelligent and dedicated working man lakini mafisadi weshamzidi kete. Si haki kuona kuwa natural resources zetu zinakuwa taken na hawa mafisadi wachache wakati wananchi wetu wanaishi katika hali kama hizi. Mafisadi, rudisheni hayo mabilioni yaende yakasaidie Watanzania wenzenu.

  Kama mimi ningekuwa Rais ningewaamuru mafisadi wote waende wakakae wiki moja katika hiyo nyumba ili waone how it feels.

  Kikwete - we are behind you on this. Safisha serikali yako na asante kwa kuwajali wananchi wako hasa hawa masikini who have nothing. It means a lot to us as human beings and as Tanzanians. May God bless our beautiful Tanzania inayotafunwa na wajanja wachache!

  ReplyDelete
 3. Kikwete hana lolote hapa zaidi ya kufanya usanii. Amekwenda Msoga kwa sababu kuu mbili. Mosi, ni kwao. Na pili ni kuwateka watu kisaikolojia. Ni wangapi wanagongwa tena jijini Dar es salaam tokana na mipango mibovu ya barabara ya serikali yake na haendi kuwajulia hali? Kesho mtamsikia akituma salamu za rambirambi Moshi ambako mwanamke kichaa aliua watoto wake watatu ilhali hali hii inasababishwa na serikali chovu na chafu kutowaweka vichaa kwenye sehemu maalumu kama ilivyo kwenye nchi za magharibi.
  Watanzania acheni huruma za kipumbavu. Rais kushiriki kwenye msiba kijijini kwake ni aina fulani ya ukabila na upendeleo.
  Rais mwenye kutimiza wajibu wake hana muda wa kufanya hivyo kutokana na wingi wa majukumu muhimu kuliko la kifo.
  Badala ya kushughulika na sakata la mgomo wa wafanyakazi na angalau kutimiza ahadi moja anapoteza muda kwenye mambo madogo!
  Matondo nilikuomba unitumie physical address yako nikutumie SAA YA UKOMBOZI. Sijasikia toka kwako kulikoni mwanawitu?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU