NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, May 12, 2010

TAHAJUDI (MEDITATION) - TAALUMA INAYOENDELEA KUKUA KWA KASI

 • Taaluma na falsafa ya tahajudi-meditation sasa imekubalika hata katika nchi za Kimagharibi. Hata madaktari wameanza kuwashauri wagonjwa wao kufanya meditation kama sehemu ya tiba, mazoezi ya kimwili pamoja na kuleta utulivu wa kifikra na kisaikolojia. Katika viwanja vya ndege vingi, kwa mfano, sasa kuna vyumba maalum ambamo wasafiri waliochoka wanaweza kuingia na ku-meditate kabla ya safari zao.
 • Hapa ni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O'Hare kule jijini Chicago nchini Marekani. Nilipoiona picha hii nilimkumbuka Kamala

4 comments:

 1. Hii taaluma sasa imeanza kuingia hata ambako haikuonekana kufaa. Imeanza kutumika hata katika kupunguza VURUGU kwenye jela zilizo na wahalifu hatari zaidi hapa Marekani.
  Niliwahi andika kuhusu hili (http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/04/nguvu-ndani-mwetuyenye-u-siri-wa.html)na kwa hakika yaonekana "kushika kasi" saana sasa.
  Baraka kwako Kaka

  ReplyDelete
 2. Hii kitu nzuri....

  ... Lakini kama kila kitu kizuri kama vile hata Makanisa ya Kilokole, ... utastukia makanisa yanaongezeka mpaka ya uongo kwa kisingizio kilekile cha KUOKOA.

  Au tu kama MADAWA MBADALA siku hizi Hapa kwetu Bongo.:-(

  Hii kitu siku hizi inapata sifa kuanzia maswala ya ngono mpaka jinsi ya kuishinda mashine ya kucheki nani anadanganya(polygraph)... na naamini ukihitaji kuna atakaye kufunza meditesheni zisaidiazo unogewe na chakula kilichochacha.:-(

  ReplyDelete
 3. siku nzima ya jana nilijifungia sehemu kwa ajili ya hii kitu, acha kabisa.

  suruhu la kila jambo

  ReplyDelete
 4. nafurahi sana kusoma kuwa kuna watu huku tz wanajua kuhusu na wanajifunza tahajudi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU