NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, May 20, 2010

"TATIZO" LA NGUO ZA MITUMBA; NA TULIKOTOKA

 • Kama nguo kama hii inavaliwa katika jamii ambayo haifahamu lugha iliyotumiwa, basi hakuna neno. Sidhani kama huyu mama na wanajamii wenzake wanafahamu ujumbe ulio katika fulana hii. Inawezekana pia kwamba pengine fulana hii imevaliwa kwa makusudi ili kuwasilisha ujumbe fulani. Nimeshawahi kuona mabinti hapa Marekani wakiwa wamevaa kaptula fupi zenye maandishi yasemayo "Self Service" makalioni. Hii pia yaweza kuwa ni, kama wasemavyo wenyewe, "fashion statement!" kama huyu mdot.com hapa chini.

 • Mheshimiwa Salim Ahmed Salim "alituokoa" alipochukua uwaziri mkuu baada ya Morani kuanguka enzi zile na kuruhusu nguo za mitumba. Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba katika sehemu nyingine za nchi watu walikuwa wameanza kuvaa nguo za magunia. Tumetoka mbali ati!

6 comments:

 1. Mwaka 2005 nikiwa Ipinda Kyela, nilikutana na brathameni mmoja kavaa fulana imeandikwa 'sex instructor, first lesson free'

  Nina wasiwasi kama alielewa maana ya maandishi yale.

  ReplyDelete
 2. Enheee! Hapo umelenga. Mara nyingi tunafanya vitu bila kujua madhara ama maana ya tukifanyacho...lol!

  Nahisi hata weye Prof. uliamua kuwa mtaalamu wa Isimu bila kujua kuwa kuna baadhi watakushangaa kama weye unavomshangaa huyo mama...lol!

  Ngoja nipate michembe kidogo si unajua msimu wenyewe ndo huu?

  ReplyDelete
 3. ni kweli. kwa miaka yoote aliyoishi duniani, na tokea aanze vitendo hivyo, lazima ni star kweli kweli. maana kama ni vimwago alivyowahi kumwaga basi hata tank kuubwa la maji linajaa, so ni star kiukweli kweli

  ReplyDelete
 4. kati ya vitimbi vya namna hii nilivyokutana navyo ni kijana mmoja wa kiume kutinga tisheti imeandikwa 'i am a tomboy'

  ReplyDelete
 5. Kamala nawe....Mwache mama wa watu aserebuke na fulana yake.

  Ng'wanambiti - tungejua madhara ya kila kitu tukifanyacho kabla ya kukifanya mbona tusingeweza kuishi? Tusingelala, tusingekula, tusingezaa, tusinge...

  Mimi simshangai huyu mama kwani naamini hili ni tatizo la lugha tu. Kama hajui kilichoandikwa katika fulana yake hakuna tatizo. Hata kama anajua lakini hakimhusu, kuna tatizo? Isitoshe pengine kuwa porn star ni kazi yenye heshima katika sehemu zingine hapa duniani. Unajua inachukua muda na juhudi kiasi gani mpaka mwanamke "mrembo" aweze kubahatika kupigwa picha na kutokea katika gazeti la Playboy na mengine ya aina hiyo?

  Mwaipopo - Nimeshawahi kuona mabinti hapa Marekani wakiwa wamevaa kaptula fupi zenye maandishi yasemayo "Self Service" makalioni. Na nikiwa kule Honolulu Hawaii nilimwona jamaa amevaa sare ya gerezani yenye viherufi vidogodogo "I am a" vikifuatiwa na miherufi mikubwa myeupe F.A.G. Watu walikuwa wanamshangaa lakini jamaa wala alikuwa hajali.

  ReplyDelete
 6. Olá;

  Obrigado!!!
  BRAZIL!!

  www.pecadosdamesa.com.br

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU