NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, May 7, 2010

TOFAUTI KATI YA WAKURYA NA WAJITA


Nilianza kiuchokozichokozi na kimzahamzaha tu hivi.....

NB: Tofauti ya Wakurya na Wajita ni ipi? Wajita ni wapole lakini Wakurya ni wakali sana. Wajita ni wavuvi (si wavivu?) lakini Wakurya ni wafugaji. Nyingine???

********************
Nikajibiwa hivi......
 1. Wajita ni karibu na Wakerewe na Wakara...Wazinza, Wahaya, Wahangaza. kusema kweli majina mengine ya mahali huko sehemu za Burundi, Rwanda, na Uganda Kusini na Kusini Magharibi ni sawa na sehemu nyingine za Majita: Bulinga, Buinja!
 2. Wakurya wanachonga meno na kutoboa masikio; wako karibu na Wazanaki, Waikizu, Wanata, Waikoma, Wangurwimi (Wangoreme), na Wasimbiti.
 3. Wakurya ni karibu na makabila ya Bonde la Ufa: Wakisii, Wakalenjini, Wamaasai, Waturkana wa huko Kenya na makabila mengi ya Tanzania ya Bonde la Ufa, kwa mfano, Watatoga, Wambulu na kadhalika. Niseme ni  mchanganyiko wa Wabantu na Wanailotiki.
 4. Ninaamini Wajita ni Wabantu zaidi ukilinganisha na Wakurya!
 5. Wajita wako Musoma na Wakurya wako huko Tarime.
 6. Ni mwiko kwa Wajita kutahiri wasichana wao.
 7. Wajita wengine hawatahiri wavulana wao, pia.
 8. Wajita si wachunga ng'ombe sana (wakulima na wavuvi) kama Wakurya.
 9. Wajita hawatoboi masikio.
 10. Wajita hawachongi meno.
 11. Wajita hawadai mahari ya ng'ombe wengi kama Wakurya, kiasi cha vijana wao kujihusisha na wizi wa ng'ombe.
 12. Wajita walikumbatia elimu ya kisasa zaidi kuliko Wakurya.
 13. Wajita walipeleka vijana wao mashuleni kuliko Wakurya waliopenda wavulana wao kuchunga ng'ombe na wasichana wao kuthaminiwa kwa mahari kuliko elimu ya mashuleni.
 14. Wajita ni akina yego (wanaume) na yebhe (wanawake); Wakurya ni akina mura wanaume na mukari (wanawake).
Kibwagizo: Nahene!
Hili ni jibu la mdau makini wa blogu hii anayejiita Esteemed Reader. Kuna cha kuongeza hapa? Mzee wa Mataranyirato upo?

4 comments:

 1. Wakurya ni mabinamu wa Wakisii...lol!

  Wakurya: wnawake huwowa wanawake a.k.a nyumba ntobhu wakati kwa wajita mila hiyo haipo!

  Wakurya: ndoa za utotoni zi tele na posa yaweza kutolewa hata mtoto akiwa mimba bila kujua jinsi yake

  Wakurya: elimu kwa mtoto wa kike si muhimu saana kama kwa mtoto wa kiume!

  Wakurya: mwanaume ama kijana wa kiume asokuwa na kovu la ngeu ama panga anasemekana ana sura ya kidemudemu (mwanamke) na ukiwa na ngeu/ngeo kwa kucharangwa na panga,kisu ama rungu wewe ni mwanaumeeee!

  Kamala na Koreo watamalisia mengine...lol

  ReplyDelete
 2. Wakati wa ukoloni, kulikuwa na makabila kama 14 hivi katika Mkoa wa sasa wa Mara.

  Makabila hao yalianza kujulikana zaidi nchini wakati wa enzi za kupigania uhuru. Jina la Julius Kambarage Nyerere lilipanua ufahamu wa makabila hayo.

  Kuna pia kutoyaelewa vizuri makabila ya Mara! Kwa mfano, watu wengi huwa wnafikiria kuwa makabila yote ya Mara ni ya hao "mura" na wengine wote ni Wajaluo. Picha hii ni ya kawaida hasa katika majeshi yetu (polisi na ulinzi).

  Wengine huwa wanasema kuwa Mkoa wa Mara ni kabila moja tu, kama walivyo Wachagga japo huko u-Chaggani kuna Wamarangu, Warombo, Wavunjo, Wakibosho na Wamachame.

  Lakini huo mfano u-Chaggani hauwezi ukafunikwa juu ya makabila ya Mkoa wa Mara. Kwa mfano, Wajita na Waruri/Wakwaya ni tofauti kabisa na makabila mengine yaliyo karibu na Wakurya.

  Waruri/Wakwaya nao wanatumia neno, mbani, wakati wakuongea (wanaume), kama walivyo Wakurya na wenzao wa karibu. Lakini Wajita hawatumii hilo neno; wanatumia yegho/yebhe (ki-jinsia), kama ilivyoelezwa na wengine.

  Na hata kabila la Washashi/Wasizaki haliko karibu na makabila mengine yaliyo karibu na Wakurya. Washashi/Wasizaki ni mchanganyiko pengine wa Waikizu na Wasukuma!

  Esteemed Reader

  ReplyDelete
 3. Wajita wengi nao wana koo mbali mbali. Kama walivosema hapo juu Wajita wako pia wabantu na pia kushi hasa wale wanaotoka koo ya Rusori ambao pia ni wafugaji na ni warefu sana na pia weupe ingawa wengine wengi ni weusi kwa Sasa kulingana na muingiliano.
  Kama ilivoelezwa hapo juu Wajita wengi wana asilia ya Rwanda, Burundi na Uganda na pia Nubian na Hausa Pia. Hii inatokana na kutazama koo zao na nyingine zafanana na Bunyoro, Butoro hata kwa lugha Kuna maneno wanaelewana.

  ReplyDelete
 4. Lugha ya kijita ni dialect na kinyarwanda, nyambo, toro, banyoro, Chiga, Zinza, kihangaza, kerewe, kihaya, Kikara(wakala pia wanatokea kusini mwa Sudan na pia Ethiopia) na kadhalika.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU