- Kama tungepunguza ukubwa wa dunia na kuifanya iweze kukaliwa na watu 100 tu huku uwiano wa watu uliopo sasa ukibakia ule ule, mambo yangeonekana kama ifuatavyo:
*******
- Watu 57 wangetoka bara la Asia
- Watu 21 wangetoka bara la Ulaya
- Watu 8 wangetoka bara la Afrika
- Watu 52 wangekuwa wanawake
- Watu 48 wangekuwa wanaume
- Watu 70 wangekuwa si weupe (wazungu)
- Watu 30 wangekuwa weupe (wazungu)
- Watu 70 wangekuwa si Wakristo
- Watu 30 wangekuwa Wakristo
- Watu 89 wangekuwa "heterosexuals"
- Watu 11 wangekuwa mashoga na wasagaji
- Watu 6 wangemiliki asilimia 59 ya utajiri wote wa dunia, na wote sita wangetoka Marekani.
- Watu 80 wangeishi katika makazi duni
- Watu 70 wangekuwa hawajui kusoma na kuandika
- Watu 50 wangekuwa wanasumbuliwa na utapiamlo
- Mtu 1 angekuwa anakaribia kuiaga dunia
- Mtu 1 angekuwa anakaribia kuzaliwa
- Mtu 1 tu angekuwa amesoma mpaka chuo kikuu
- Mtu 1 tu angekuwa na kompyuta
- Chanzo: Jones, Laurie B. 2004. Teach Your Team to Fish: Using Ancient Wisdom for Inspired Teamwork. Three Rivers Place.





Hii inafikirisha sana
ReplyDeleteKaazi kwelikweli!
ReplyDeleteKaribu tena Kaka.
ReplyDeleteKaribu saaana