NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, June 19, 2010

MH. MALECELA NA UMASIKINI WA WATANZANIA

 • Hapa chini ni kauli ya Mheshimiwa John Malecela aliyoitoa tarehe 6/6/2010 kule wilayani Kahama alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Jamii Vijijini (VICOBA). Yuko sahihi?
****************************

Akizungumzia umasikini miongoni mwa Watanzania, alisema Tanzania hakuna umasikini wa kumfanya mtu alale na njaa na kusubiri kufa.

Alisema kama kungekuwa na watu wa aina hiyo, nchi isingekuwa na amani na utulivu kama ilivyo sasa.

“Mtu hawezi kukubali kufa njaa, vinginevyo ataenda kuvunja nyumba ya mtu ye yote ili apate chakula na hapo ndipo mwanzo wa kutoweka kwa amani,” alisema.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi la tarehe 8/6/2010 (Ukurasa wa 10)

****************************

4 comments:

 1. Yuko sahihi kwa kuwa hawa majambazi na vibaka wanaotusumbua mpaka kunakuwa na kanda maalumu za kipolisi wamekosa chakula :-(

  ReplyDelete
 2. huyu jamaa amelewa na ufisadi wa ccm, kama dodoma tungepata wabunge kama mo dewji tungekuwa mbali, lakini huyu alikuwa mbunge toka mkoa wa dodoma tangu uhuru,kwa hiyo mkiona wagogo wanakuja kuomba dar ni kwa sababu ya huyu na job lusinde,simon kimwaga, hawa jamaa wanajifikiria wao.

  ReplyDelete
 3. sidhan kama atakuwa serious, lakini si haba ndani ya land cruizer v8, akishuka ndani ya ukumbi wenye AC, na nyumabani kuna AC, sidhani kama anaendaga kijijini kwao.....! maana nina uhakika kila mtanzania ana ndugu fukakara. "asirudie tena kusema hivyo atapta laana itakayodumu hata kwa vizazi vyake".

  ReplyDelete
 4. These guys never die na kupisha wengine. Duh! Nimemsoma huyu mzee kwenye somo la siasa wakati nikiwa darasa la nne enzi zile na mpaka leo tu bado anadunda. Ndiyo maana yuko out of touch na maisha halisi ya Mtanzania wa kijijini. Hebu aende akamwambie haya maneno Mgogo mwenzake Matonya tuone atampa jibu gani.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU