NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, July 17, 2010

ILI KUONDOA MIKANGANYIKO, WAKATI MWINGINE NI BORA "KUJITAMBULISHA"

 • Juzi nikiwa katika duka la Walgreens, nilikutana na jamaa ambaye naamini kabisa alikuwa ni mwanaume japo alikuwa amevaa gauni safi na kujipodoa sawasawa. 
 • Nikiwa naangalia mashine ya kunyolea ndevu, huyu "jamaa" alinisogelea na kuanza kuniambia kwamba alikuwa amevutiwa na shati langu (kikoi cheupe chenye ramani ya Afrika ikiwa imepambwa na wanyama mbalimbali). Alitaka kujua ni wapi angeweza kupata shati kama hili. 
 • Japo sina tatizo na watu kujibadilisha jinsia zao, unapokutana na mtu aliyefanya hivyo kwa njia ya operesheni na/au matumizi ya homoni kidogo unaweza kushangaa. Pamoja na kwamba huyu jamaa alikuwa "mwanamke mzuri" kwa umbo, bado unaweza kuiona asili yake ya kiume katika sauti, sura na hata mwonekano wa miguu na mikono yake. Ndiyo maana namfagilia sana huyu jamaa hapo juu kwa kuweka mambo bayana namna hii. Dunia hii we acha tu!
  *******************
  • Kwa habari zaidi kuhusu masuala haya bofya hapa.

  4 comments:

  1. Huyo atakuwa alizaliwa mwnaume kwa bahati mbaya sana........
   Kuna jambo najiuliza hivi zama za manabii watu wa aina hii walikuwepo, maan nasikia Sir Eltone John alidai kuwa hata Bwana Yesu aliufagilia ushoga, nimejitahidi kusoma Biblia lakini sijakutana na ukurasa wenye maandiko hayo...labda wana utambuzi hasa Kamala, Kaluse na Chacha watueleze kama kiutambuzi ushoga unaangukia wapi, ni kizalia au ni kasoro kama vile ulemavu na kadhalika?

   ReplyDelete
  2. Nakuunga mkono Koero kwa swali lako kwa hawa wanautambuzi. kuna wakati hili jambo linachanganya akili hadi nahisi kucnganyikiwa. huyu Elton ni jitu ambalo siku zote linataka kupotosha mambo. sijui alikusudia watu wauheshimu ushioga wake ama la kwa ksuema hata yetu alikuwa akifagilia inaleta shida kiasi kikubwa. pamoja na kujitambusha kwa huyu bwana bado naamini kasoro kubwa ya wanadamu ni ukosefu wa kuthibti uhuru wao. kila ukitazama aina sheria zilizopo tunaambiwa huo ni uhuru binafsi. lakini kwa hakika natamani sana tungekuwa kama nchi za kiiislamu kuhusu hawa mashoga. ni mtzamo tu huu

   ReplyDelete
  3. Markus, Hatuna haja ya kuhitaji sheria za kiislamu kwa sababu hata huko kwenye nchi za kiislamu kuna tatizo kubwa la mashoga, utumiaji wa mihadarati pamoja na kwamba wale wanaokamatwa na mihadarati hukatwa vichwa hadharani......
   hili ni tatizo kubwa nadhani ina haja ya kuliangalia kwa jicho la ndani na ndio maan nikaomba msaada wa wanautambuzi...

   ReplyDelete
  4. Koero nimesoma changamoto yako, naomba unipe muda nitaifanyia kazi.
   Tupo pamoja

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU