NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, July 30, 2010

KIKWENU MNAHESABUJE? KIKWETU KUNA NAMBA ZA KIKE (BAKIMA) NA ZA KIUME (BAGOSHA)


17 comments:

 1. kikwetu tunahesabu 1,yimonga, 2,yivili, 3,yidatu, 4,mcheche, 5,muhano.... halafu ett, ni moja två mbili, tre 3, fyra 4, fem 5:-)

  ReplyDelete
 2. Yasinta - hiki SIYO kikwenu...ett, ni moja två mbili, tre 3, fyra 4, fem. Japo umeolewa na hawa jamaa, KAMWE hutakuwa kama wao. Daima likumbuke hili. Hata wakupende vipi but you will always be BLACK and they will always be WHITE...And you will always be MNGONI....

  ReplyDelete
 3. Naomba ufafanuzi: Kwa hiyo inamaana namba za KIUME ni zakutumiwa na WANAUME tu?

  ReplyDelete
 4. Mtakatifu Simon;

  Kama umeshajaribu kujifunza hizi wanazoziita Romance Languages (mf. Kifaransa, Kihispania, Kiitaliano na Kireno) utakuwa umegundua kwamba huko nomino (na pengine maneno mengineyo) zimegawanywa katika mafungu mawili kulingana na jinsia: feminine na masculine.

  Kinachoshangaza hata hivyo ni kwamba matumizi ya nomino hizi hayajali wala kuzingatia jinsia hizi katika ulimwengu halisi (Lugha inazungumzwa na kila mtu ati!.) Wataalamu sasa wanadhani na kuamini kwamba hata ngeli za majina katika lugha za Kibantu pengine zinaweza kuangaliwa kama zilivyo "gender markers" katika lugha zinginezo. Kwa kifupi ni kwamba; ni rukhsa kutumia namba zozote zile bila kujali jinsia.

  ANGALIZO: Kutokana na athari za kitamaduni,lugha nyingi huwa "zinapendelea" sifa za kiume (mf. umeshawahi kujiuliza ni kwamba mwanamme peke yake ndiye huoa katika Kiswahili na mwanamke yeye huolewa?). Kwa mantiki hii hii hata katika Kisukuma, mfumo wa kuhesabu wa kiume ndiyo hasa unachukuliwa kuwa ndiyo mfumo wa jumla. Kwa hivyo ukiniamsha usiku wa manane na kuniambia nianze kuhesabu kwa Kisukuma, nitahesabu kwa kutumia namba za kiume - solo, bili, yatu.....

  Swali: Mtakatifu, unajua kuhesabu kwa Kipare???

  ReplyDelete
 5. Da yasinta: kumbe wewe ni chotara? yaani una lugha 2? mbona ile ya tatu hukusema?


  1. kamwe, 2. kabherhe, 3. katato, 4 kane, 5. katano, 6. kasansabha, 7. muhungate, 8. monane, 9. kenda, 10. ikomi!!!

  Kwa kawaida kikwetu namba saba ni balaa kama ilivyo namba 13 kwa wasungu....lol!

  ReplyDelete
 6. Duuuh namba za kiume na kike? sie twahesabu 1.yimwi 2.sivili.3.sidatu.4.sihanu.5.sitai.6.sita.7.saba.8.tisa.10.kumi.Natumaini nitakuwa nimepatia nitamuuliza mama, kama nitakuwa nimekosea then nitarudi kusahihisha.

  ReplyDelete
 7. somo zuri sana. vipi kuhusu viitikio vya kiswahili vya 'naam' na 'abe'

  ReplyDelete
 8. Weee Edna!!! Ukichumbiwa utarudi kumuuliza mama kama ukubali ama ukatae? si unajua jibu? Acha utani hebu muache mama tupe majibu usijidai hujui kinyumbani TUTAKUTENGAAAA...LOL!

  ReplyDelete
 9. Edna - kweli hata kuhesabu tu mpaka ukamuulize mama??? Hebu muulize mama tuone. Nina wasiwasi sana na namba 5, 6, 7, 8 na HASA tisa. Nyingi kati ya hizi ukimuuliza mama nategemea kwamba zitakuwa tofauti....Ni lugha gani hii?

  ReplyDelete
 10. 1. Wak 2. Tsar 3. Tam 4. Tsiyah 5.Koan 6.Lahhoo 7. Fangw 8. Dakat 9. Gwalel 10. Mibangw

  ReplyDelete
 11. Malkiory - hiki ni Kiiraqw au lugha gani hii? Nilikaa pale Mbulu kwa mwezi mmoja hivi na nakumbuka mengi tu. Nilipapenda!

  ReplyDelete
 12. Ni kiiraqw bwana Matondo. Kumbe ulikuwa hujui kama mimi ni Mwiraqw! Mbulu ulitembelea miaka ya nyuma kidogo bila shaka. Mji mkongwe ambao ulizinduliwa siku moja na jiji la Nairobi. Lakini akina Marmo wameizamisha kwenye dimbwi la umasikini. Nikuambie kuwa nikitaka kuwatumia wazazi wangu hela ya matumizi ni lazima waende Babati ambao mtu itamlazimu kushinda pale hadi siku inayofuata ndipo arejee nyumbani. Wazazi wangu wanaishi karibu kilomita kama 40 toka Mbulu, hivyo ingekuwa rahisi kwa wao kumtuma mtu wa kwenda na kurudi siku hiyo hiyo pale Mbulu. Lakini cha kushangaza ni kwamba, western union ya Mbulu ipo tu kwa jina. Ukienda kuchukua hela pale hata Shilingi laki moja hawana kwenye balance pamoja na kuwa Mbulu ni makao makuu ya wilaya tena wilaya kongwe. Kichekesho kweli kweli.

  ReplyDelete
 13. Kweli hapo kuna tatizo. Bariadi kwa Mzee wa vijisenti ni Wilaya pia lakini pale Western Union unaweza kuchukua hadi milioni moja bila wasiwasi wo wote. Ukitaka kuchukua zaidi ya hapo ndiyo watakwambia uende mkoani Shinyanga au Mwanza.

  Tatizo la baadhi ya hawa wanasiasa wetu ni kuyaona majimbo wanayoyawakilisha kama mali yao binafsi. Nilipokuwa Arusha hivi majuzi nilishangazwa na kitendo cha Mheshimiwa Anne Kilango kumlalamikia Kapteni Makamba (tena bungeni kabisa!) kwamba eti kuna watu wanalizengea JIMBO LAKE la Same Mashariki na eti Makamba hafanyi lolote kuwapiga stop. Ni mtindo huu unaofanya watu wanakuwa wabunge kwa zaidi ya miaka 40. Ndiyo maana nilifurahishwa na hekima ya wazee akina Mzindakaya na Kimiti kuamua kupumzika kwa hiari yao wenyewe. Watu tumewasoma kwenye somo la siasa wakati ule tuko darasa la nne (akina Kingunge, Makweta, Malechela...) lakini mpaka leo bado wanapeta tu. Na ukienda huko majimboni mwao mambo ni yale yale. Mbulu ni ya Phillip Marmo na itabidi msubiri mpaka atakapoamua kupumzika mwenyewe (kumbuka kwamba hawa jamaa wanaishi marefu kweli!)

  Phillip Marmo amewahi kuwa naibu spika wa Bunge huyu. Basi mtu ungedhani kwamba angelipa kipaumbele jimbo lake kimaendeleo kumbe wapi. Sijui...

  ReplyDelete
 14. Matondo, Tanzania inaelekea pabaya kwa sasa, kuna kila dalili tusipokuwa makini nchi itadumbukia kwenye utawala wa kurithishana kama kweli kwenye nchi za falme za kiarabu n.k Hivi sasa watoto wa vigogo ambao baadhi yao wazazi wao wamekuwa viongozi kwa takribani miaka 30 wameanza kuoneka wazi kwenye anga za siasa wakati wazazi wao bado madarakani, hii mimi kidogo inanipa wasiwasi,Ukiangalia kwa undani vigezo vya kurithishwa uongozi wanazo, sababu wazazi wao waliweza kuwapeleka Uingereza, Marekani na kwingineko kupata elimu ya uhaki. Angalia mtoto wa Kikwete ni kada wa CCM, binti wa Pinda ameshinda ubunge kwa kishindo na mtoto wa Makamba kwa vyovyote vile pia atashinda. Japo ni haki yao kikatiba kuchaguliwa lakini nalo suala la uchu wa madaraka linajionesha hapa ukizingatia wazazi wao bado wako madarakani.

  ReplyDelete
 15. kaka matondo nadhan i Edna ni muhehe si unajua wao niwatani:-)

  ReplyDelete
 16. Yasinta - mwache Edna ajitetee mwenyewe. Likizo yako inaendeleaje?

  Malkiory - Ukiangalia vizuri hata mfumo wetu wa elimu una lengo lile lile la kuhakikisha kwamba watoto wa tabaka fulani ndiyo wanapata elimu bora zaidi ya watoto wa wakulima. Sera yetu ya lugha ya kufundishia ni mfano mzuri kuthibitisha dai hili.

  Ngoja tuone tunakoelekea lakini mimi sikushangaa kuona kwamba Karume mwingine alikuwa anagombea uraisi kule Zanzibar....

  ReplyDelete
 17. Jamani Chacha,Masangu ndio mmenishambulia hivyo?Asante Yasinta Mtani wangu, Mimi ni mnyalukolo original...Kama nilivyoorodhesha hizo namba hapo juu ni ukweli mtupu.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU