NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, July 21, 2010

KWA MNAOTANGAZA NIA. MMESHALISIKIA HILI?

 • Inasemekana kwamba mbali na kuwa na mamilioni ya kuwahonga wapiga kura, inakubidi sasa uwe na "mtaalamu" bingwa wa kukulinda. Vinginevyo kampeni yako haitafika popote! Na mwenyewe ukizubaa eti unaondoka. Kauli hizi nilizisikia sana kutoka kwa wapiga kura kule Usukumani hivi karibuni. Sijui hali katika sehemu zingine za nchi ikoje!

 • Kuzidi kuimarika kwa imani hizi za kishirikina katika jamii yetu kidogo kunashangaza. Mbona hali inazidi kuwa hivi wakati ambapo tuna shule za msingi kila kijiji, shule za sekondari kila kata, akademi kila "mtaa" na vyuo vikuu lukuki? Lengo la elimu yetu ni nini hasa kama siyo kutukomboa kutoka katika umasikini, ujinga, maladhi na dhuluma kama Baba wa Taifa alivyotuahidi enzi zile? Mbona utandawazi unaonekana kushindwa kuziangamiza imani hizi za kishirikina wakati unaonekana kufanikiwa kuvipiga dafrau vipengele vingine vya utamaduni wetu kama vile lugha zetu za mama, ngoma za kiasili, mavazi na mfumo wetu wa maisha kwa ujumla? Kwa nini ushirikina unazidi kujiimarisha? Tufanye nini?

6 comments:

 1. Labda ungeangalia ni kundi gani linalong'ang'ania madaraka na kuendesha hizo kampeni kwa sasa. Ni wale wale ambao wengi wao wametokea enzi za ukoloni!! Je hizo shule, vyuo vikuu na akademi zimeanza lini? Tayari zimeshatoa matunda ya kutuwezesha kutoangalia mambo kama ya kishirikina? Kwa mtazamo wangu ni kwamba bado tuko njiani na hatutofika hivi karibuni. Safari ni ndefu na hiki kizazi kinachong'ang'ania madaraka inabidi kipite kwanza. Tunahitaji muda...

  ReplyDelete
 2. Matondo khs suala la ushirikina jamii yetu bado
  inauamini sana,mimi huwa nabishana na watu mara
  kwa mara ninapopinga imani za kishirikina.
  Kuna kipindi mkuu wangu wa kazi alizuia tusiwapeleke wanafunzi field katika kijiji kimoja
  ambacho yeye alidai kuna ushirikina,staff yetu ina
  wahitimu zaidi ya 15 wa chuo kikuu lakini tulioto
  fautiana na mkuu tulikuwa wawili tu na tulishindwa!
  Kwa hiyo imani hizi za giza hazitaisha labda
  hadi tutakapoupanga upya mfumo wetu wa elimu,hata
  mauaji ya albino yanasababishwa na wanajamii
  kuamini ushirikina

  ReplyDelete
 3. ushirikina, ni suala siriasi hili japo naona kama viongozi wa dini wanapaswa kulaumiwa kwa haya zaidi, japo ni vigumu kutenganisha dini zetu na ushirikina

  ReplyDelete
 4. Mnaziita zile shule za Sekondari shule? Mimi naziita majengo ya kata. It is a joke kuziita shule. Ukweli ni kwamba hatuko siriazi. Kama mawaziri wenyewe wanapishana Bagamoyo kwa wataalamu, watu wa kawaida unategemea wafanye nini? Na hii biashara ya maalbino unafikiri ni ya watu wadogo hii?

  ReplyDelete
 5. HABARI MATONDO MAKALA ZAKO NAZIPENDAGA SANA JE; USHIRIKINA MAANA YAKE NININI?MBONA WAZUNGU WANAUME KWA WANAUME WANAOANA JE HUO SI USHIRIKINA?AU WEWE UNASEMAJE? HATA MAMBO YA KUTAMBIKA NI UTAMADUNI SIO USHIRIKINA LABDA YULE ANAYE UA ALBINO AU KUMTOA MTU KAFARA KWELI HUYO NI {}INGAWA SIJAILEWA MAANA YA USHIRIKINA.WAZUNGU NI WASOMI LAKINI WANAFANYANA WANAUME KWA WANAUME HAPO VIPI

  ReplyDelete
 6. Mfalme Mrope - ni kweli pengine muda bado. Lakini kinachonishangaza mimi ni ukweli kwamba sekta zingine za utamaduni wetu zinaandamwa sana na utandawazi lakini si ushirikina. Pengine ni umasikini wetu lakini napo inatetwa kwamba biashara hizi za ajabu ajabu kama viungo za maalbino zinaendeshwa na watu wenye pesa. Kweli bado safari ni ndefu.

  Munale - mfano wako haushangazi. Kama imani za kishirikina ni sehemu ya utamaduni wetu, na kama elimu yetu imetusaidia kuulinda utamaduni wetu, basi hili ni jambo jema. Hata kama hivi ndivyo, bado kuna ulazima wa kuzitathmini upya tamaduni zinazotupeleka ndiko-siko. Nilitegemea kwamba utandawazi ungeusukuma ushirikina pembeni lakini sivyo.

  Kamala - viongozi wa dini wapi walaumiwe? Dini zetu za jadi au zile za kutoka Ulaya? Kwa nini?

  Anony wa kwanza - kweli shule zingine za kata pengine hazistahili kuitwa shule. Kuna moja niliiona ina walimu wawili tu - hakuna maabara wala maktaba. Sijui kinachosomwa pale ni nini.

  Anony wapili. Asante kwa kupenda makala zangu ingawa kusema kweli muda wa kuandika kwa makini haupo. Ni kweli wazungu pia wana ushirikina wao ingawa wa kwao pengine siyo "dramatic" kama huu wa kwetu wa kuua maalbino. Bado wanaamini katika kusoma alama za vidole kwa kutumia nyota. Ingawa wanaita ni sayansi lakini mimi sioni tofauti na Msukuma anayekwenda kupiga ramli kwa daktari wa kienyeji. Nawajua wazungu ambao hawafanyi jambo lolote bila kwanza kusoma utabiri wa nyota zao unasemaje.

  Kuhusu mashoga kuoana wao kwa wao sina uhakika kama huu ni ushirikina. Inasemekana kwamba ushoga ulikuwepo/upo katika jamii nyingi za Kiafrika ingawa ulikuwa (bado) unafanyika kwa kificho.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU