NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, July 27, 2010

MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI YATAPATIKANA LINI?


 • Picha hizi nilizipiga mwenyewe nilipokuwa nyumbani Usukumani mwezi wa sita mwaka huu. Hapa ni kijiji cha jirani na wanakijiji hawa huwa wanapata maji yao kutoka katika kisima hiki ambacho pia nadhani hutumiwa na mifugo pia.
 • Ni kweli tumeshindwa kuchimba visima na kuhakikisha kwamba watu wetu wanapata maji safi na salama? Tutaulaumu umasikini wetu hata katika jambo la msingi kama hili mpaka lini? Nilishawahi kutoa dukuduku langu kuhusu suala hili hapa.

3 comments:

 1. Kaka Matondo: tatizo si umaskini bali na jinsi tunavyoyaangalia mambo kimtizamo hasi zaidi ya chanya.

  Hii imetujengea usugu na utegemezi kwamba hakifanyiki kitu mpaka sirikali ilete ama mnene wa mjengoni idodomia alete. tumeuza uhuru wetu na kuwakabidhi fisi/simba watulindie!!!

  ReplyDelete
 2. Huu ndio muda muafaka wakuwauliza hawa wanaoitwa viongozi najua majibu wanayo na ya kutia moyo lakini kama inawezekana ni bora kuandikishana mbele ya wanasheria, au mnasemaje

  ReplyDelete
 3. Ng'wanambiti - na hicho ndicho kioja - simba wanapokabidhiwa (au tuseme wanapojikabidhi) mwanambuzi wa maendeleo yetu. Inakera na kuumiza moyo mtu unapoona binadamu kama wewe wanahangaika kupata huduma za msingi kama hizi na wakati watu wanaotakiwa kuwasaidia na kuwaonyesha njia hawajali.

  emu-three - kwenye kura mambo ni yale yale tu hakuna jipya. Pea za kanga na baisikeli zitawasahaulisha watu machungu yao. Na safari ya kutoenda popote itaendelea

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU