NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, July 13, 2010

NI KWELI HATA KWA JIHAD???

 • Ni katika maandamano ya kudai mahakama ya kadhi hivi karibuni. Binafsi nina wasiwasi sana na haya maneno ya mwisho katika hili bango!

2 comments:

 1. CCM wanafanya utani na hawa jamaa. Wanadhani kila mtu ni wa kuchezea. Leo wanaandika. Kesho watafanya wanayoandika. Halafu CCM hiyo hiyo ndiyo itakuwa ya kwanza kulaani maadui wa "umoja na mshikamano"

  Hawa jamaa waelewe (japo najua hawataelewa) kuwa suala la Mahakama ya Kadhi linawahusu wao wenyewe. wasitake kuchanganya imani zao na haki za wengine. Kama walikubali kudanganywa na CCM basi wakamalizane na CCM hiyo hiyo kwenye sanduku la kura mwezi Oktoba!

  ReplyDelete
 2. Kuna watu ambao hawajui madhara ya vita na pengine hawajawahi hata kuisikia AK 47 ikiunguruma au bomu likikata miili ya watu huku na huko. Mimi ni masikini lakini niacheni na umasikini wangu na mniachie amani yangu. Jihad tumeona madhara yake. Mnapojifunga mikanda na kuripua watu wanaoangalia kombe la dunia kama kule Uganda, maana yake nini??? Mbona msiende na kujaribu kumripua Museveni, mawaziri na hata wabunge? Akiuliwa mbunge, kiongozi au mwanasiasa kwangu mimi ni sawa kwani hawa jamaa wameshakula vya kutosha lakini Jihad kwa watu wasio na hatia - masikini tu kama nyie it is not acceptable kabisa.

  Kama ni CCM imewaudhi nendeni mkapambane nayo wenyewe. Kama hamjui Makamba anakoishi njoni niwaonyeshe ili mkampelekee hiyo Jihad mwenyewe lakini IACHENI AMANI KATIKA NCHI YETU iendelee. Au ionyesheni CCM kindumbwendumbwe mwezi wa 10 wakati wa uchaguzi.

  Halafu watu wa CCM nao wamekaa kimya tu wakiangalia vitisho hivi vikitolewa. Siku mabomu yakianza kuripuka pengine ndiyo wataamka. Itapendeza kama nini kama yataanza kuwaripukia wao wenyewe. Pengine wataamka mapema zaidi. MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU