NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, July 28, 2010

NI KWELI KUNA DAWA ZA KUNENEPESHA MAKALIO YA WANAWAKE (AKA MCHINA) AU NI POROJO TU ZA KIBONGO?

 • Profesa mmoja wa "Medical Anthropology" ambaye hufanya utafiti wake nchini Tanzania aliniomba nimletee sampuli ndogo ya dawa za kunenepesha makalio ya wanawake ambazo alikuwa ametajiwa tu na mwanafunzi mmoja kutoka Tanzania. Aliniambia kwamba anataka kwanza kuzifanyia uchambuzi wa kisayansi ili kufahamu kemikali zilizomo katika dawa hizo (kama kweli zipo!).
 • Mbali na kuandika makala mengi ya kiutafiti kuhusu tiba za jadi katika makabila ya Kusini mwa Tanzania, utafiti wa sasa wa Profesa huyu unajaribu kuangalia athari za utandawazi katika tiba hizi za jadi ambazo zimedumu kwa miaka mingi miongoni mwa Waafrika.
 • Nilipokuwa Tanzania mwezi wa sita mwaka huu nilijaribu sana kuzitafuta dawa hizi lakini sikufanikiwa. Nilikwenda katika maduka ya madawa karibu matano lakini kote niliambiwa kwamba hata wao walikuwa wanazisikia tu. Hata baada ya kujitambulisha na kueleza lengo langu la kuzitafuta dawa hizo, majibu yalikuwa ni yale yale. 
 • Ni kweli dawa hizi za kunenepesha makalio ya wanawake zipo au ni porojo tu za Kibongo? Kama kweli zipo, kuna anayejua kama kuna uchanganuzi wo wote wa kisayansi ambao umekwishafanywa kuhusu kemikali zilizomo katika dawa hizi na madhara yake kwa binadamu? Nitawezaje kupata japo sampuli kidogo tu? Matone au mabonge machache tu yanatosha.
******************************
Angalizo: Hata hapa Marekani, nasikia vuguvugu la mabinti "kujijaziajazia" lipo lakini inasemekana wenyewe wanafanya operesheni kabisa. Binti katika picha hiyo juu ni modo mashuhuri kule jijini New York na inasemekana kuwa amefanyiwa operesheni. Kazi kweli kweli!

5 comments:

 1. pengine yapo na pia ya kuongeza ukubwa wa uume ngoja tufanye ufukunyungu!

  Fikra zetu zukiwa kengeufu ndipo unapopata visa kama hivi :-(

  ReplyDelete
 2. Hata mimi nilikuwa na hamu sana ya kupata ukweli huo, na wengi wamesema dawa hizo zipo labda wataalamu na serikali ingetoa tamko na kukemea kwani madhara yake hayataonekana leo, ila baada mtu keshafikisha miaka 40s,.
  Sawa, labda mpitie kidogo nilichoandika kuhusiana na mada hii:
  http://miram3.blogspot.com/2010/07/usione-vyaelea-vimeundwa.html

  ReplyDelete
 3. Kaka Matondo dawa hizo zipo kabisa. Nilizungumza na dada mmoja mwezi uliopita akanisimulia juu ya dawa hizo. Nikipata nafasi ya kukutana naye tena nitamwona maelezo kwa kirefu zaidi. Ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar.

  Anasema dawa hizo ni za Kichina. Huletwa na wafanyabiashara kutoka China. Anasema zipo kama lotion. Hivyo mhusika hupaka maeneo yale anayoyahitaji yaumuke. Na kama utakosea kupaka, si ajabu kuona kalio moja kubwa kuliko jengine.

  Kina dada hapa Dar hususani wanafunzi wa vyuo wanaelezwa ni watumiaji wazuri wa hizo dawa. Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, dawa hizo huuzwa kuanzia shilingi elfu hamsini na kuendelea. Hivyo kwa maelezo yake, huchangishana hata watu wawili ama watatu na kununua.

  Nilimuuliza kama aliona mabadiliko kwa watumiaji, akaniambia mabadiliko huja tena kwa siku chache.

  Nadhani hukuweza kuzipata kwa kuwa ulitafuta kwenye maduka ya tiba asilia.

  Lakini wapo wahusika tena wakiwemo watu maarufu wanaotajwa kuwa waagizaji wakubwa. Tena sambamba na kukuza makalio pia zipo za kurudisha bikra.

  Mji hapa kaka kila kitu kimechakachuliwa.

  ReplyDelete
 4. Kaka Matondo dawa hizo zipo kabisa. Nilizungumza na dada mmoja mwezi uliopita akanisimulia juu ya dawa hizo. Nikipata nafasi ya kukutana naye tena nitamwona maelezo kwa kirefu zaidi. Ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar.

  Anasema dawa hizo ni za Kichina. Huletwa na wafanyabiashara kutoka China. Anasema zipo kama lotion. Hivyo mhusika hupaka maeneo yale anayoyahitaji yaumuke. Na kama utakosea kupaka, si ajabu kuona kalio moja kubwa kuliko jengine.

  Kina dada hapa Dar hususani wanafunzi wa vyuo wanaelezwa ni watumiaji wazuri wa hizo dawa. Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, dawa hizo huuzwa kuanzia shilingi elfu hamsini na kuendelea. Hivyo kwa maelezo yake, huchangishana hata watu wawili ama watatu na kununua.

  Nilimuuliza kama aliona mabadiliko kwa watumiaji, akaniambia mabadiliko huja tena kwa siku chache.

  Nadhani hukuweza kuzipata kwa kuwa ulitafuta kwenye maduka ya tiba asilia.

  Lakini wapo wahusika tena wakiwemo watu maarufu wanaotajwa kuwa waagizaji wakubwa. Tena sambamba na kukuza makalio pia zipo za kurudisha bikra.

  Mji hapa kaka kila kitu kimechakachuliwa.

  ReplyDelete
 5. Bwana Fadhy - hebu livalie njuga suala hili nipate angalau sampuli kidogo tu. Nitashukuru sana!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU