NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, July 15, 2010

"VITUKO" VYA MTAA WA MAKOROBOI JIJINI MWANZA (NA KWINGINEKO). KULIKONI ???

  • Niliipiga hii picha tarehe 7/6/2010 pale mtaa wa Makoroboi jijini Mwanza. Kuna maduka mazuri sana ya nguo na vifaa mbalimbali lakini katikati kabisa ya maduka haya ndipo kuna "kituko" hiki. Naona manispaa wameweka tu hili "karandinga" la kukusanyia uchafu halafu wakalitelekeza na kuingia mitini.
  • Tabia hii ya kuanzisha miradi (tena mingine mizuri sana) na halafu kuitelekeza tunayo sana. Utakuta mkandarasi kapewa barabara kisha anajenga kakipenda kadogo tu halafu huyo anatokomea. Na hapo mabilioni ya shilingi za walipa kodi yanakuwa yameshatafunwa. Mifano ya jambo hili ni mengi sana na ni mojawapo ya tabia za kizembe ambazo inabidi tuzipige vita kama kweli tunayo nia ya dhati ya kusonga mbele. Ni kweli manispaa ya jiji la Mwanza haina uwezo wa kuja kuzoa uchafu huu na kuupeleka kunakotakiwa kwa muda uliopangwa kabla haujarundikana namna hii? Au ni uzembe tu na kutojali? Halafu kipindupindu kikifumuka eti tunaanza kulaumiana!
  • Kwingineko nilivutiwa sana na juhudi za usafi zinazofanywa katika jiji la Arusha na hasa katika mji wa Moshi. Huko sasa mtu mpaka unaona aibu kutupa ganda la chungwa hovyohovyo. Tatizo hata hivyo ni kwamba bado kuna upungufu wa mapipa ya kutupia takataka. Pale Arusha inabidi utembee na ganda lako la chungwa kwa muda mrefu kabla hujaona sehemu ambayo unaweza kulihifadhi. Hata hivyo hatua nzuri zimepigwa na kwa mara ya kwanza kuna dalili za kweli kuonyesha kwamba watu wenyewe wameanza kubadilika kiasi kwamba mtu unaona aibu kutupa ganda la chungwa hovyo hovyo. Haya ni mabadiliko chanya na hili ni jambo jema!    Tovuti ya Manispaa ya Arusha inapatikana hapa.

2 comments:

  1. Hala utakuta mtu aliyekabidhiwa kazi hii anakuja kazini asubuhi na kurudi nyumbani bila wasiwasi. Mpaka ajitokeze mfadhili ndipo takataka zitazolewa...

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU