NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, August 27, 2010

FIKRA YA IJUMAA: ARGUMENTUM AD HOMINEM

 • Argumentum Ad Hominem ni dhana muhimu katika taaluma ya Lojiki na Mantiki. Dhana hii hutumiwa kuelezea mashambulizi au hoja ambazo zinaelekezwa kwa mtu binafsi (mf. mwanasiasa) badala ya kumakinikia kile akisemacho (mf. sera zake). Pengine mifano bora kabisa ya Argumentum Ad Hominem niliwahi kuigusia hapa na hapa
 • Ingefurahisha kama nini kama wakati huu wa uchaguzi tungeacha kuwashambulia wagombea binafsi na badala yake tukamakinikia sera zao kombozi kwa jamii. Ati, kati ya wagombea wote wa urais, ni yupi mwenye sera zenye mashiko na zinazotekelezeka? Ni yupi ambaye ana uchungu na maisha ya Mtanzania wa kawaida? Ni yupi ambaye ameonyesha moyo wa kizalendo na kutetea sera zake kombozi, hata kama kwa kufanya hivyo imebidi afarakane na maswahiba wake? Yupi ni kiongozi bora ambaye ataisadia Tanzania kusimama kidete na kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania??? Kiongozi wa aina hii ndiye tunayepaswa kumchagua.
 •  Tuogopeni ARGUMENTUM AD HOMINEM kama ukoma!
Wikiendi njema

2 comments:

 1. Na ndipo Watanzania tunapokosea, badala ya kuangilia `nini tunatafuta' tunaangalia `ni nani tunamtafuta'
  'Wanasemaje vile, simple mind discuss people and complex mind discuss events...' kwa wanaumombo wanajua zaidi yangu.
  Wakati umefika wakujua nini tunachokitaka, halafu tuangalie ni nani anaweza kutupatia hayo matakwa yetu, na hayo tutayapata kwenye sera zao, kwasababu akichaguliwa mtu hatungi sheria zake, anachotekeleza ni sera alizoziainisha awali.
  Jaribu kutafiti na kuwauliza Wadanganyika au Wazenji-bara, sera gani anazozijua ambazo zimeanishwa kwa mgombea anayemtaka,...utasikia yule ataleta udini, yule ataleta ukabila, e hivyo vimeandikwa kwenye hizo sera zao?

  ReplyDelete
 2. leo ni miongoni mwa siku nimeshibishwa taaluma. hicho ulichokisema profesa ndicho kinachotokea sasa. kwa mfano mgombea mmoja ameanza kuandamwa eti amemwacha mke wake wa zamani na kuoa mwingine. sasa hili linatuhusu ninikatika uhalisia wake?

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU