- Kwa nini tulipigwa/tunapigwa/(tutapigwa) viboko kwa kuzungumza lugha zetu za mama, jambo ambalo kimsingi ni haki yetu ya kibinadamu? Kwa nini tuadhibiwe kwa kuzungumza lugha yetu ya taifa? Kwa nini tulazimishwe kuzungumza lugha tusiyoifahamu na ambayo hatukuandaliwa vizuri kuifahamu? KWA NINI???
mawasilianoikulu
1 week ago




Mimi naamini mfumo mzima wakufundisha watoto Bongo unaendana na adhabu , viboko na kutishana.
ReplyDeleteUkifuatilia watoto wafunzwavyo chochote kile unaweza kustukia watoto wengi tu wabwengwao hata makonzi kwa vitu ambavyo wangeambiwa tu.
Na hata ukifuatilia mafunzo yalivyowakilishwa hata jandoni na unyagoni lazima vitisho sana na mkong'oto hapo hata kabla ya kukatwa ngozi ya mbele ya utupu au kukeketwa bila ganzi.
Kwa hiyo hii STAILI YA UFUNZAJI si ajabu ilijitokeza tu mahali pengine na ndio maana utaikuta ilijitokeza mpaka mashuleni
Nilivyofika FINLAND miaka hiyo nilishangaa kukuta tokea miaka hiyo watawaliwe na Waswedi bado walikuwa wanalazimishwa kusoma Kiswidi kwa lazima. Kwa hiyo hii kitu haiko BONGO tu ingawa FINLAND mkong'oto haukuwepo ingawa kila aliyedhamiria kujulikana msomi alijua lazima pamoja na Kifini inabidi ajua na Kiswidi kama anataka kula bata kwa mrija kilaini.
Sababu ni MOJA NA NDOGO
ReplyDeleteWanaopanga mfumo wa uelimishaji ni WATUMWA WA KIAKILI
Hawana mawazo chanya wala mawazo yao binafsi. Hawawezi kuwa kama "transit" ya mawazo kisha wakawa na yale yatufaayo kwani "source" ya mawazo yao ni ambako kunahangaika kutwa-kucha kututawala
Baraka kwako
NAWAZA KWA SAUTI TUU!!!!!!!!!!!
Hatuja patu waziri anaye husika na elimu aliye makini na anajuwa wajibu wake katika swala zima la elimu.nasema hivyo kwa sababu kama waziri anakuwa anajuwa nini umuhimu wa lugha ya kiswahili kwa taifa la Tanzania kunge kuwa na utaratibu unaoeleweka katika nini kifanyike kati ya kiswahili na kiingereza.kutokujuwa kiingereza siyo huna akili nikwamba hujuwi lugha hiyo basi.kwa hiyo ukipigwa kwa kuzungumza kiingereza ni ubabe wa wakufunzi wetu.hawajuwi walitendalo. kaka s.
ReplyDeletewewe, si elimu ya mkoloni? ni lazima tujue kidhungu, una wabongo kibao marekani, unafikiri bila mkongoto wa kidhungu mgeenda huko?? si mgekuwa usu-kumani?
ReplyDeleteelimu yetu ni ya kitumwa na hatuwezi kuibadili haki ya nani sijui
Katelefoni! Katelefoni! Please don't smoke my river!!
ReplyDelete