NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, August 20, 2010

FIKRA YA IJUMAA: MASHARTI HAYA YA VIONGOZI YALIKUWA MTEGO WA RUSHWA???

Angalizo: siungi mkono rushwa lakini naomba tuliangalie swala hili kwa jicho la kibinadamu huku tukizingatia hulka na mahitaji ya binadamu kama mnyama!
**************
  • Masharti ya viongozi kama yalivyoainishwa katika Azimio la Arusha yanasema hivi:
VIONGOZI

1. Kiongozi wa TANU au wa Serikali sharti awe mkulima au mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la kibepari au kikabaila.

2. Asiwe na hisa katika makampuni yo yote.

3. Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au kibepari.

4. Asiwe na mishahara miwili au zaidi

5. Asiwe na nyumba ya kupangisha.
***************
  • Kimsingi kilichokuwa kinasisitizwa hapa ni kwamba, ili mtu aweze kuwa kiongozi (wa ngazi ya juu), ilikuwa lazima awe masikini. Kwa hulka ya binadamu wa kawaida (ukitoa akina Mother Thereza, Mahatma Gandhi na wengineo), umasikini na madaraka vinagongana. Wanasaikolojia wengi wanasema kwamba lengo la binadamu ni kujiendeleza na kujipatia uwezo wa kujipatia mahitaji yake katika viwango mbalimbali kwa urahisi.  Kama hivi ndivyo; ni wazi kwamba ni vigumu sana kwa mtu masikini kupewa madaraka makubwa mf. uwaziri au ukurugenzi wa shirika la umma na asiitumie nafasi hiyo kujiendeleza yeye na familia yake.  
  • Maswali: Lojiki ya masharti haya ya TANU ilikuwa ni nini? Je, hawa viongozi walitakiwa kuwa watakatifu na kuzikana hulka zao za kibinadamu? Masharti haya yalisaidia kuchochea rushwa kwa viongozi hawa masikini kuanza kuiba kisirisiri?
  • Katika nchi nyingi zilizoendelea, huwezi kugombea nafasi ya juu kama uko masikini; na nafikiri mfumo huu pengine unasaidia kuzuia hizi rushwa za mara kwa mara ingawa nao pia, (kutokana na uchoyo na tamaa) wanaiba na kula rushwa.
  • Mwisho: Masharti haya yalikuwa ni mtego usioepukika kwa viongozi hawa masikini?Ungekuwa wewe ungeuepuka?

1 comment:

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU