NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, August 29, 2010

USHINDI UNAKUJA ATI!


Inaonekana CCM wamefanya "kufuru" kwa kununua "nyuso" hizi za magazeti ili kujitangaza. Ukiwa na vijisenti vyako haliharibiki neno ati! Kama nilivyosema jana, wapinzani kazi mnayo! Picha ni kutoka kwa Mjengwa.

5 comments:

 1. Kama watanzania wataamka pesa hata wanunue vyombo vya habari vipi haziwezi kusaidia. Wenzao wa KANU walikuwa na ndoto za mchana kama hizi. Mwisho wa siku walijikuta pakanga. Nadhani tatizo la Tanzania ni kuwa na baadhi ya wapinzani wanaotumiwa na CCM. Hivi ukiondoa Dr Silaha, waliobaki wanatafuta nini iwapo watu kama Lipumba walishajaribu na kuishia pakavu kama si kuisaidia Chama Cha Mahabithi?

  Hata hivyo sitamshangaa sana Lipumba maana dhumuni la kuanzishwa CUF lilitimia hivi karibuni Seif alipokaribishwa ulaji Zenj and that is that.

  Kama watanzania wataendelea kujirahisisha na kuwa vyangudoa ni juu yao. Hebu angalia yule mama mwenye NGO ya kutia mashaka ya WAMA anavypiga kampeni kwa ajili ya CCM mchana kutwa akiitumia WAMA ile ile. Au ni yale yale ya ujambazi wa Anna Mkapa? Ama kweli wadanganyika ndio waliowao.

  ReplyDelete
 2. Mwalimu Mhango. Usemacho pengine ni kweli. Ni wazi kwamba Mrema ni CCM na ametumiwa vizuri sana kuua upinzani. Hamadi hali kadhalika. Mabere Marando pia. Makongoro Nyerere na wengineo. Sasa baadhi ya hawa watu ndiyo wanakimbilia tena CHADEMA. Hakuna kitakachoendelea huko. Ndiyo maana mimi nilikuwa CHADEMA lakini baada ya kuona mambo yanayoendekea huko nimeamua kurudi CCM ammbako afadhali wako wazi na sera zao. Slaa peke yake hataweza cho chote and at the end of the day ataachwa peke yake tu.

  Ukweli ni kwamba HAKUNA chama cha upinzani chenye ubavu wa kuitikisa CCM kwa sasa. Hata Slaa mwenyewe mimi simwamini na I won't be surprised kama naye ni CCM. Ilikuwaje mke wake agombee through CCM na baada tu ya kutemwa eti ndiyo anakimbilia CHADEMA.

  CHADEMA bado kuna akina SHIBUDA na vibaraka wengineo. Masikini Tanzania my country...

  ReplyDelete
 3. Pamoja Tutashinda, ushindi ni lazima. Si pesa si nini ni maandalizi na kuwa na mikakati ya maana. Huwezi kushiriki uchaguzi ikiwa hujajiandaa utaishia kulalamika kila siku. Ruzuku ya vyama mwaka 2010 imefikia bilioni 17, zimefanya kazi gani?

  Na utashindaje uchaguzi ikiwa badala ya kuandaa wagombea wako unasubiri makombo kama fisi? Nyie mlioko nje ambao hamkushiriki chaguzi za serikali za mitaa ndo mtajidanganya kuwa Dr. Slaa au Chadema atashinda wapi? Watu hawana hata matawi ya chama watashindana na chama chenye mashina? Mbali na hayo tumechoka na sera ya ufisadi, tunataka tuone sera za maana, ya kusema nitapunguza ukubwa wa serikali huku unasema utaleta mfumo wa serikali tatu, hii ya tatu itakuwa hewa?

  Mwisho hiyo yaweza kuwa kazi ya Chief Marealle guru wa PR mzee wa Solutions, kada na kamanda wa vijana wa ccm. Ni suala la kujipanga tu maana tangu 2005 ilijulikana 2010 kutakuwa na uchaguzi.

  ReplyDelete
 4. Ruzuku bilioni 17? That is a lot of money hata kama ni za wafadhili.

  Vyama vya upinzani bila shaka vimegawana hiyo ruzuku. Si unajua vinaendeshwa kama miradi ya watu binafsi. Halafu hawana hata aibu eti wanakemea ufisadi.

  Hata tulioko nje tunajua kwamba wapinzani hawana chao kwani hata CHADEMA ni miyeyusho tu. Hata ofisi za wilaya hakuna sasa watashindaje? Helikopita???

  Halafu Slaa naye ni bonge la disappointment. Msomi namna ile atajikanganyaje kwa kudai eti atapunguza ukubwa wa serikali wakati huo huo anaunda serikali ya Tanganyika - jambo ambalo mwalimu Nyerere alilipinga kwa nguvu zote?

  Wapinzani watalalamika tu lakini they are no better than anybody. Ruzuku zinamilikiwa na wenyeviti na makamu wao wakati vyama vinazidi kudorora. Zingetumika kuimarisha matawi ya wilayani, kata na tarafa leo pengine vingekuwa na uhai. Instead wanagombana na hawaishi kukimbia vyama wakitafuta maslahi. Eti hawa ndiyo wanataka kuongoza nchi. NO WAY na kwa mtindi huu CCM itakaa madarakani for many decades to come!!!

  ReplyDelete
 5. SLAA NI BOMU. ETI ATAPUNGUZA UKUBWA WA SERIKALI KWA KUFUTA MANAIBU WAZIRI NA WAKUU WA MIKOA. SO FAR SO GOOD

  HALAFU ETI ATAUNDA SERIKALI YA TANGANYIKA...SO WHICH IS WHICH??? Kufuta manaibu waziri na wakuu wa mikoa kutasaidia nini kama tena unaunda serikali ya Tanganyika??? This flawed analysis real shocked me and changed my views of him. I will not vote for this man!!!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU