NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, August 5, 2010

HUU NDIO MKOA WA SHINYANGA NG'WANAWANE !!!

 • Ni mkoa mzuri sana wenye utajiri mkubwa wa madini, mifugo na maliasili zinginezo.
 • Lakini pia ni mkoa wa mwisho kielimu kwa miaka mingi sasa.
 • Ni mkoa ambao wakazi wake wana imani kali na dhati katika ushirikina.
 • Kwa hivyo ni mkoa unaoongoza kwa mauaji ya vikongwe
 • Hata mikasa hii ya Jidulamabambasi na Shibuda (kama ni kweli), kama ule wa waziri Mgeja wakati ule, si ajabu ikahusishwa na mambo ya ushirikina.
 • Jisomee hapa na hapa.

4 comments:

 1. Si ndio mkoa huu huu ambao kuna kile kijiji maarufu cha ghamboshi. Kijiji ambacho unaweza kukiona hicho hapo lakini waweza kutembea siku nzima bila kukikuta.( ndivyo nisikiavyo). Ucku kijiji hiki ati kinaonekana kimejengeka vizuri kama New York vile. Haya ni ya kweli? Nasikia tu kwa watu.
  Yote ya yote, huu ndio mkoa wa Shinyanga.

  Labda niulize tu serikali ina mkakati gani wa kuondoa uteja huu wa kushika mkia kwa mkoa wa Shinyanga ktk nyanja ya elimu (swali la nyongeza muheshimiwa waziri).

  ReplyDelete
 2. Gamboshi nimeshafika na kukaa na sikuona cho chote. Mimi nadhani ni porojo tu hizi. Ni kijiji masikini sana ambacho hakina cho chote....

  ReplyDelete
 3. Kama Jidulamabambasi kafa ghafla na Shibuda kapata "stroke" basi huko Shinyanga wallahi hakukaliki. Mimi napendekeza watu waliofanya hivyo wakatwe mapanga tu...

  ReplyDelete
 4. Hili ndio tatizo la nchi yetu, mkoa unazalisha miwa kwa ajili ya sukari, lakini sukari hiyo ikishazalishwa inapeleka Dar, ndipo mgawo uanze. Mimi ningeona ule utwala wa kiuchumi wa majimbo ungefaa utumike kwa mfano mko kama huo unaozalisha madini kinachpatikana kwa madini hayo kitumike kwanza humo, na ziada ndipo ipelekwe kwingine, kwasababu upungufu wa elimu unachangiwa pia na umasikini

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU