NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, August 23, 2010

KWELI YOTE HAYA NI KWA AJILI YA SIMU? KUNA TATIZO KATIKA JAMII YETU

Huyu "kibaka" eti ALITUHUMIWA kumwibia simu abiria mmoja aliyekuwa kwenye daladala lililokuwa likitoka Tandika kuelekea Mwenge.
 ************
(1) Raia mwenye hasira akimtwanga tofali


(2) Kijana hoi bin taabani


(3) Baadaye anafumbua macho na kuomba msaada

(4) Mgambo wanafika na kumwokoa

 • Kama nilivyosema katika maoni yangu kuhusu jambo hili katika blogu ya Pwani Raha, hili si jambo la kufurahia. Hii ni dalili wazi ya ndwele angamizi na nyemelezi ambayo inatutafuna kimya kimya huku tukijinadi kwamba tunaishi katika nchi ya amani. Watu wana hasira na ipo siku hasira hii itaripuka tu tutake tusitake. Tatizo ni kwamba wamiliki wa mfumo wanaonekana kutojali, pengine kutokana na ukweli kwamba wanaosulubishana kwa hii staili ya haki ya papo kwa papo ni walalahoi kwa walalahoi. 
 • Walalahoi hawa wakiamka siku moja na kuacha kubondana matofali wao kwa wao; kisha waelekeze hasira zao kwa wamiliki wa mfumo itakuwaje? Historia inaonyesha kwamba hatua hii ikifikiwa, hakuna jeshi hapa duniani linaloweza kurekebisha mambo. Tujihadhari!
NYONGEZA
Kibaka mwingine huyu hapa akichomwa moto!!!

 • Picha zote ni kutoka Global Publishers
Nyongeza

Tukio la hivi karibuni kule Musoma

11 comments:

 1. kwa kweli binadamu tuna roho za ajabu binadamu mwenzako unamtupia mawe kama alikuwa nyoka????

  ReplyDelete
 2. 'Hivi nyie hamna huruma na binadamu wenzenu' mama mmoja akasema, siku mbili baadaye akaibiwa mkufu wake wa dhahabu, unajua alichosema, siku nimkamata mwizi na mchoma moto.
  Ukiibiwa kitu chako cha thamani utaona ubaya wa mwizi, lakini hasira sizigeuke hasara, dawa ya mwizi sio kumuua au kumchoma moto...
  Kuua au kuchoma moto nihasira ya ndani kwa ndani kama moto ndani ya majivu, ipo siku utalipuka na wanyonge wadai haki yao inayopotea, hivi sasa hawajui ni nani anayiiba hiyo haki , ndio maana ukiikota jiwe unamtupia mwizi, unadhani ndiye aliyekupa huo umasikini!
  Ole wenu siku haki akiamua kujitokeza na kumsema nani aliyekuwa akimficha siku zote!

  ReplyDelete
 3. Wewe unayemponda mawe mwana wa mwenzio bila hata ya chembe ya huruma ,ungejisikiaje kama angekuwa ndugu yako,mtoto wako ndiye anayepondwa mawe?

  ReplyDelete
 4. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu. Fikirieni kua ingekua ni wewe umeibiwa unafikiri ungechuka hatua gani katika kujihami na simu au chotechote ulicho ibiwa! Kwa kweli inatia uchungu mtu kubondwa au kufanyiwa unyama wa namna huo.Lakini tukurudi nyuma, haya matukio ya mtu kufanyiwa hivyo siyo mageni kwa wahalifu wanao fanya hivyo, imekua ni mazoea kwao na wanajua fika ipo siku au za mwizi ni 40 atakuja umbuliwa mitaani kama ilivyo mtokea jamaa huyo. Tatizo wamezoea hawa watu, vipi utamuibia mwenzako simu hujui amenunua kwa gharama gani, kwanini usifanye kazi nawe ununue yako. Inatakiwa tuangalie huko na huko kupata jibu muafaka,,, lakini nao wamezoea hao,,, ngoja apone uone kama hawezi kuja kukuibia na wewe hapo ndio utakuja ona uchungu wake, si ajabu wakati atakapo kuibia na atakapo shikwa na wasamaria wema si ajabu wewe ndio utakua wa kwanza kumbonda na mawe,,,

  ReplyDelete
 5. Kaka Matondo: Nanukuu "Walalahoi hawa wakiamka siku moja na kuacha kubondana matofali wao kwa wao; kisha waelekeze hasira zao kwa wamiliki wa mfumo itakuwaje? Historia inaonyesha kwamba hatua hii ikifikiwa, hakuna jeshi hapa duniani linaloweza kurekebisha mambo. Tujihadhari!"


  I wish hasira hizo zingeanza na mwaka huu kwenye sanduku la kura!!!

  ReplyDelete
 6. Anonymous wa 4:38 PM - Kila sehemu hapa duniani kuna vibaka lakini pia kuna polisi na mahakama. Vyombi hivi vina kazi gani basi kama watu wanabondana matofali namna hii kwa KUTUHUMIANA kuibiana simu? Ndiyo maana nikasema kuna tatizo katika jamii yetu.

  Mimi huwa sijisikii vibaya jambazi lililoua watu linapohukumiwa hukumu ya kifo mahakamani. Lakini hii ya kuua mtu eti kwa vile tu umemtuhumu kwa kukwapua simu yako (hata kama iwe ya gharama namna gani!), sikubaliani nalo. Sitanyanyua tofali hata siku moja kubonda kichwa cha mtu aliyenikwapulia simu!

  Mfumo ni mbovu, polisi wanapendelea, mahakamani hakuna haki, maisha ni magumu, watu wana hasira.....

  ReplyDelete
 7. Kwa mara nyingine nakubaliana na Mkuu Masangu Matondo Nzuzullima katika pointi yake ya mwisho.

  ReplyDelete
 8. Umasikini uliokithiri ndiyo chanzo cha udokozi. Fikiria kama mtu huyo aliyeteswa hivyo na hatimaye kuuawa pengine hakuwa na chakula! Je kitendo cha kumhukumu kwa adhabu kali kama hii siyo dhambi hata mbele za mungu.

  Napingana na mauaji haya ya kikatili kwa wadokozi wa vitu vidogo vidogo kama vile simu, saa, cheni za shingoni n.k,

  Kwa upande mwingine sina kipingamizi na mauaji ya wahalifu wakubwa, mfano, majambazi wanotumia silaha za moto kufanya uhalifu wa mali na raia. Japo pia napinga kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mikononi.

  ReplyDelete
 9. Na huyu ANATUHUMIWA tu. Tukumbuke kwamba mtu akikosea akakupigia makelele ya mwizi mwizi basi kimbembe unacho! Utaishia kupondwa matofali UKITUHUMIWA kuwa kibaka. Watu hata hawaulizi umeiba nini ali mradi tu wamesikia makelele ya mwizi mwizi basi ni kuuliwa na kuchomwa moto! Jamii gani inayofanya hukumu kwa njia hii. Vipi baadaye ikijulikana kwamba hukuiba kitu lakini UMETUHUMIWA tu lakini tayari ukawa umeshauawa? Ni nani anabeba lawama? Haki iko wapi?

  Kwa kumwangalia huyu kijana hali yake inatia huruma na kusikitisha. Pengine tuanze kuwabonda matofali mafisadi waliotuibia mabilioni (sijui yanaweza kununua simu ngapi?) badala ya kubondana sisi kwa sisi walalahoi.

  Siku ya kesi ya Mramba, Mgonja, Chenge na Yona wananchi tuzuke pale mahakamani na Matofali kama haya tuone itakuwaje. Kalagabaho Tanzania!

  ReplyDelete
 10. Hata yule aliyekorofishana na rafikie kisa msichana na kupigiwa kelele za mwizi na watu kumvamia na kuanza kumpiga na kisha kumtia petroli!! Si haki, Kazi hizi ziachiwe vyombo vya dola.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU