NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, August 8, 2010

MAHINDI BEI POA LAKINI ......................

 • Jana nikayaona haya mahindi mabichi yakiuzwa kwa bei poa kabisa: mahindi 10 kwa dola 1 na senti 49 tu!
 • Tena unaweza kuchagua kama unataka ya rangi ya njano kama hapo juu

 • Au meupe kama unapenda.
 • Tatizo hata hivyo ni kwamba ukiyapika au kuyachoma, mahindi haya hayana ladha kabisa kama yale niliyoyazoea kutoka Bariadi Usukumani. Ni kama vile tu unatafuta karatasi. Bila shaka yamelimwa "kisayansi" kutokana na mbegu zilizohandisiwa kisayansi. Yaani ni vurugu tupu.
 • Juzi tu Waingereza wamegundua kwamba nyama ya ng'ombe waliozaliwa kwa kutumia njia hizi za kisayansi ilikuwa inauzwa madukani na sasa wanapiga makelele kweli
 • Japo hakuna anayejua hasa madhara ya kula vyakula hivi, kuna wasiwasi mkubwa sana kwamba vyakula hivi huenda vikawa vinasababisha matatizo makubwa ya kiafya yakiwemo mfumuko wa aina mbalimbali za saratani na magonjwa mengine yanayoathiri moyo pamoja na viungo vingine vya ndani na hata ubongo. 
 • Kinachoshangaza ni kwamba, katika juhudi zetu za kuendana na usasa, wakazi wa mijini (wenye pesa zao) kule nyumbani sasa wanaona fahari kwenda kununua mahitaji yao mengi katika "masupamaketi" yaliyoenea kila kona. Sijui kuna faida gani kununua nyama iliyotoka Afrika Kusini katika supamaketi badala ya ile ya ng'ombe aliyetoka Usukumani hapo katika bucha ya jirani? 
  • Jana nilipika mahindi manne na leo bado naendelea kuhangaika na haya sita yaliyobakia. Kazi ninayo!

  No comments:

  Post a Comment

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU