NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, August 19, 2010

MAMA YUPO KWENYE NDEGE, MTOTO ANALIA, MAMA KABEMBELEZA KACHOKA, AKAAMUA KUMZABA MTOTO KIBAO, ABIRIA WAKALALAMIKA...SASA ENDELEA

 Picha hii iko hapa.

****
...mfanyakazi wa kwenye ndege akamchukua mtoto,
Baada ya ndege kutua polisi wakaitwa,
wazazi wakahojiwa,
wakaonekana ni wazazi wazuri,
Wakaachiliwa na kuruhusiwa kuendelea na safari yao,
Na "ishu" ikamalizika.

Kuna la kujifunza hapa?

*********

Kwa habari kamili kuhusu kisa hiki soma hapa.

5 comments:

 1. Huko Ulaya bwana, nafikiri wakatimwngine wanazidisha, kwasababu mtoto kama mtoto unaweza ukamkanya kwa mdomo asisikie kabisa, na hata kukudharau, lakini ukimpa adhabu kidogo anajirekebisha na hata kuwa na kumbukumbu kuwa nikifanya hiki ni kosa nitaadhibiwa.
  'Haki ya mtoto ipo' kuwa asinyanyaswe, lakini pia anahitaji haki nyingine ya kulelewa kimaadili, na hapo ndipo hata ffimbo hutumika, usimpomnyosha leo kesho ataamua atakavyo, kama wenga wanenanvyo, samaki mkunje angali mbichi.
  Kuna mambo ya kuiga, na siyo yote yanafaa kuiga, tuangalieni msimamo wetu kwa manufaa ya vizazi vyetu

  ReplyDelete
 2. mimi sikubaliani kabisa na emu-three! kuwa ulaya wanalea watoto kama yai. Sikubalini sikubalini na sikubalini. Kwani kiboko si njia ya kumfundisha mtoto hata kama unasema mtoto mkunje angali mbichi unaweza pia kumkanya mtoto kwa maneno kwa kumwita na mkaa na kumwelekeza lipi ni jema na lipi ni baya. Sio lazima utumie kiboko. Hapo naona walezi walichoka baada ya safari walikosa uvumilivu na mtoto pia kukaa tu alichoka. Kupiga mtoto si kumfunza nakataa kabisa.ni mtizamo wangu.

  ReplyDelete
 3. Yasinta hata biblia inasema kumkanya au kumfundisha mtoto kwa kutumia kiboko.. ngoja nitafute nitarudi nikupe mistari usome.. tupo wengi tuliopata watoto wetu huku ugenini/america lakini mila na desturi ipo pale pale tusidanganyane hapa.

  ReplyDelete
 4. Viboko ni lazima. Anony wa mwisho. Nadhani unaongelea yale matoto ya nabii Samweli ambayo yalidekeshwa mpaka yakawa yanaiba kanisani. Mwishowe yakaleta maangamizi makubwa kwa taifa zima la Israeli.

  Biblia inakubali viboko na mimi naamini kwamba viboko ni lazima katika malezi ya mtoto. It will be a mistake kwa Tanzania kufuta viboko na kujump kwenye hii bandwagon eti viboko ni kumhadililidha mtoto. Mbona sisi tulipigwa sana na tumetoka OK - all of us.

  Hapa USA wazazi wana shida and one of the problem ni kutokuwepo na adhabu. Ukimfinya tu mtoto tayari eti umemuabuse. Na matoto hayo hayo yanakua hayana adabu na matokeo yake ni moral decay kwa taifa zima.

  ReplyDelete
 5. Methali 13:24,

  na

  Methali 22:15 “Ujinga hupatikana ndani ya roho ya mtoto; kiboko kitamtoa ...

  mimi ni mzazi mpya sasa, ila ninachangamoto kwani mimi siamini katika vboko. nawachukia woote walionichapa, wazazi, walezi hata walimu

  naamini katika kufundishana kama alivyosema yasinta na sio kupigana. nikiangalia jinsi kichanga changu kinavyolia wakati mwingine usiku, labda kingekuwa kikubwa ningekitwanga makofi kama ningekuwa naamini katika kupiga. ila sasa ni lazima tuubebe mzigo huu vyema kwa kuwalea na kuwaelekeza sio kwa vitisho na kusoma biblia utadhani ilitoka mbinguni

  wanaolejea biblia kuwatwanga watoto eti kwa kuwa imeandikwa mbona wanasoma agano la kale pekee?? hawajui kuwa agano la kale halikamiliki isipokuwa kuna agano jipya?? je agano jipya na Yesu mwenyewe a.k.a mwanzailishi wa ukristo vinasemaje juu ya mtoto??

  nilipokuwa bado mtoto nilisoma neno hili katika sikukuu ya mikael na watoto; matayo 13. Ndipo akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea.
  Kisha watu wakamletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono na kuwaombea. Lakini wanafunzi wakawakemea.

  14. Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao.
  Yesu akasema, "Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie; maana Ufalme wa mbinguni ni wa watu walio kama watoto hawa."

  15. Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko.
  Basi, akawawekea mikono, kisha akaondoka mahali hapo.

  kama haitoshi;

  Matayo 18
  Aliye Mkuu Katika Ufalme Wa Mbinguni
  1Wakati huo, wanafunzi walimjia Yesu wakamwuliza, ``Ni nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa mbinguni?'' 2Yesu akam wita mtoto mdogo akamsimamisha mbele yao. 3Kisha akasema, ``Nawa hakikishieni kwamba msipobadilika na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni. 4Kwa hiyo mtu ye yote anayejinyenyekeza akawa kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa mbinguni.

  5``Na ye yote anayemkaribisha mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, ananikaribisha mimi. 6Lakini kama mtu ye yote anamsabab isha mmojawapo wa hawa wadogo wanaoniamini atende dhambi, ingali kuwa nafuu kwake afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake akazam ishwe katika kilindi cha bahari.

  Je mna la kusema? je kati ya waliomsulubu na kumuua yesu, kuna watoto?? tuskubali upofu huu wa kibiblia ili tunyanyase watoto

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU