NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, August 26, 2010

MWALIMU ANASWA AKIJIANDAA KUFANYA NGONO NA MWANAFUNZI

  • Mwanafunzi asimamishwa masomo, lakini mwalimu wake aachwa akipeta
Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari ya wasichana Maswa Chacha Mussa (28) amekutwa na mwanafunzi wake wa kidato cha tatu (jina tunalihifadhi) mwenye umri wa miaka (16), wakijiandaa kufanya mapenzi.

Tukio hilo lilitokea Agosti 7, mwaka huu saa 7:45 mchana baada ya uongozi wa shule hiyo kupata taarifa kwamba mwalimu Chacha alikuwa nyumbani kwake na mwanafunzi.

Baada ya taarifa hizo, Mkuu wa Shule Msaidizi, Paschal Athanas na mwalimu wa zamu waliamua kwenda nyumbani kwa mwalimu na kumbamba akiwa chumbani kwake na mwanafunzi huyo.
Aidha, kutokana na tukio hilo mwanafunzi huyo amesimamishwa masomo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuruhusu uchunguzi kufanyika.

Hata hivyo, mwalimu wake bado anaendelea na kazi ya kufundisha kama kawaida na hakuna hatua yoyote ya kisheria ikiyochukuliwa dhidi yake.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Kamishina Msaidizi Daudi Siasi alisema kuwa baada ya tukio hilo kutokea polisi walipewa taarifa na kwenda kwenye shule hiyo ambapo mwanafunzi huyo alipelekwa kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya serikali ya wilaya ya Maswa na kuonekana kuwa alikuwa hajafanyiwa kitendo chochote na mwalimu huyo.

CHANZO: NIPASHE (25/8/2010)

1 comment:

  1. Ni mfumo dume. Ni nani ambaye hajui???

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU