NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, August 4, 2010

MWANZA KUMEKUCHA - NASUBIRI BARIADI KUONA MZEE WA VIJISENTI ITAKUWAJE....

Mchakato huo mkali uliofanyika siku ya Jumapili umesababisha kuanguka baadhi ya wabunge.

PICHANI BALOZI GETRUDE MONGELA.

JIMBO LA UKEREWE (WAGOMBEA 10 WALISHIRIKI). Balozi Getrude Mongela kawasambaratisha akina Joseph Lyato na Oswald masatu Monarch.
 
JIMBO LA ILEMELA (WAGOMBEA 7). Antony Mwandu dialo kawabwaga kiulaini washindani wake wakubwa John Buyamba na Pastory Masota.


JIMBO LA NYAMAGANA (WAGOMBEA 12). Lawrance Masha kawabwaga bila huruma John Mboje Marogoyi na Joseph Kahungwa.

JIMBO LA MAGU (WAGOMBEA 9). Dk. Festus Limbu kawachakaza Abel Busalama na Boniface Magembe.

JIMBO LA MISUNGWI. Charles Kitwanga kawaangusha Jackob Shibiriti(aliyekuwa mbunge) na Madoshi Makene.

PICHANI MBUNGE ALIYEANGUSHWA JIMBO LA BUSEGA DK. RAPHAEL CHEGENI.

JIMBO LA BUSEGA (WAGOMBEA 4). DK Titus Kamani kampiga chini DK> Raphael Chegeni aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo huku akifuatiwa na Nyandwi Msemakweli.

JIMBO LA KWIMBA (WAGOMBEA 7). Shanif Hiran Mansoor kachukuwa jimbo mikononi mwa Bujiku Sakila ambaye imekula kwake.

JIMBO LA SUMVE (WAGOMBEA 8). Richard Ndassa kapiga kachukuwa akifuatiwa na Richard Mchele.


JIMBO LA BUCHOSA (WAGOMBEA 4). DK. Charles Tizeba kalichukua jimbo akifuatwa kwa karibu na mwanaharakati Erick Shigongo, huku aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Samwel Chitalilo akiacha na sura ya mnuno baada ya kukamata nafasi ya tatu. 


JIMBO LA SENGEREMA (WAGOMBEA 4). William Ngeleja kaendelea kutamba akiwaacha mbali Kimasa Shejamabu na Joshua Shimiyu.

JIMBO LA GEITA (WAGOMBEA 6). Donard Max kakwea akiwaangusha Jacob Mtalitinya na Costantine Kanyansu.

JIMBO LA BUSANDA (WAGOMBEA 4). Lolencia Bukwimba akitetea ulaji wake vyema  mbele ya Tumaini Magesa na Abdala Mussa.

JIMBO LA NYANG'WALE (WAGOMBEA 4). Hussein Amar Gulamali kachukua jimbo kuwatumikia wananchi akifuatiwa kwa kura na Evarist Ndikilo ile hali aliye kuwa mbunge wa jimbo hilo James Msalika akiangukia pua nafasi ya tatu.


Wagombea hawa wote watalazimika kusubiri kikao cha Kamati Kuu ambacho kina mamlaka na idhini ya kufuta wagombea watakaobainika kuwa wamekiuka taratibu za chama hicho - ikiwa ni pamoja na kutoa rushwa kwa wapiga kura, jambo ambalo limedaiwa kujitokeza mara nyingi katika mchakato wa kura za maoni.


Kamati Kuu itakutana tarehe 14 Agosti.

Makala hii ni kutoka katika blogu ya Sengo.

2 comments:

  1. Mwaka huu mapinduzi yenye kuleta faraja yamefanyika ndani ya CCM kwa kuwagaragaza vigogo sugu. Sijui kinachoendelea katika jimbo la Mbulu,magazeti yamenichanganya kichwa. Baadhi ya magazeti yanasema Marmo kapigwa chini, mengine anaongoza!

    ReplyDelete
  2. ntawasiliana na wanangudu nipate kujua inakuwaje!!!

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU