NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, August 22, 2010

SAFARI HII NAONA "VIJANA" WAKO MACHO

 • Gari la Mheshimiwa lilipogoma kuwaka kipindi kile baada ya kuwekewa mafuta yaliyochakachuliwa, watu walishangaa na kulalamika kuhusu ulinzi wa Mheshimiwa. Kelele za wasiwasi kuhusu timu ya ulinzi wa Mheshimiwa pia zilipigwa baada ya gari lake kuchomoka tairi akiwa msafarani. 


 • Katika tukio hili la jana pale Jangwani naona "vijana" wako makini sana na walimdaka mapema.  Picha hii inatosha kabisa kuwaondoa hofu wale wote ambao walikuwa na wasiwasi kuhusu ulinzi wa Mheshimiwa. Poleni wanaCCM kwa mkasa huu. Nilikuweko jangwani mkasa kama huu ulipotokea mwaka 2005! 
 • Kwa habari zaidi tembelea blogu ya Pwani Raha. Tunampa pole Mheshimiwa pamoja na wanaCCM wote kwa mkasa huu. Mungu Ibariki Tanzania!

3 comments:

 1. Matondo, kumbe wewe ni CCM eeh. Nilikuwa sijui

  ReplyDelete
 2. Anony - Ni kipi kinachokufanya ufikiri kuwa mimi ni CCM? Je, kuwa mwanachama wa CCM ni kosa? Umenifurahisha.

  ReplyDelete
 3. Matondo, yaani huwezi hata kujificha kuwa wewe ni CCM. Vijana wangekuwa proper trained wangejua kwamba something is wrong pale tu Mzee mzima alipoanza kuhangaika kwa kusema "Aisee" huku akijishika usoni na kuuma meno. Hotuba ilikuwa inasomwa na mtu anapoanza kupaparika basi vijana waliofunzwa vizuri wangejua kwamba something was wrong. Basi wangemsogelea na pengine kumkalisha chini. Badala yake wanamwacha baba wa watu mpaka anatokomea mbele ya microphone yake. This is sad kwa sababu huyu ni kiongozi wa taifa na japo sikubaliani na sera zake nyingi na hasa jinsi anavyowalinda mafisadi, bado ni rais wangu na kuna mambo mazuri ambayo ameitendea nchi yangu. Sipendi kumwona akiadirika namna hii.

  Ningekuwa yeye ningefukuza madaktari wangu wote na kuajiri wapya wenye utaalamu zaidi. Ningeongezea pia Mlinzi mmoja au wawili waliosoma Saikolojia, Isimu na Body language.

  I hope kwamba he is OK na please madaktari na walinzi wake, make sure haanguki tena. God Bless Tanzania.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU