NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, August 3, 2010

SOMO LA KUJIFUNZA LUGHA ZETU LINAENDELEA: MNASEMAJE "MUNGU ASIFIWE" KIKWENU?

  • Kwa vile somo letu la kuhesabu lilinoga sana, leo tujikumbushe jinsi ya kusema "Mungu Asifiwe" katika lugha zetu mbalimbali. Naamini kila kabila lilikuwa na mungu au  miungu yake hata kabla ya ujio wa dini hizi za kigeni (Ukristo, Uislamu, Uhindu, Ubohora na zinginezo). Kwa mfano Wasukuma tulikuwa tunamwita mungu wetu Seba, Lyuba au Mulungu. 
  • Huyu hapa Bony Mwaitege na wimbo wake wa Sisi Sote akitukumbusha jinsi ya kusema 'Mungu Asifiwe" katika Kisukuma, Kiha, Kinyakyusa, Kihehe, Kikinga....Tunaweza kuiendeleza orodha hii kwa kuongezea lugha zingine kama Kingoni, Kipare, Kihaya, Kikurya na zinginezo. Tuwemo!
  • Kwingineko: Ni haki kwa wanasiasa kutumia salamu za kidini katika mikutano yao?. Eti unasikia mwanasiasa anawasalimu watu "Bwana Asifiwe". Salamu hizi kidogo mimi huwa zinanitatanisha!

1 comment:

  1. Hii hoja nzuri, kwasababu viongozi wa siasa mara nyingi wanasema `msichanganye dini na siasa' lakini inafika mahala wao ndio wa kwanza kuikoroga dini ndanii ya siasa, hii ni kumaanisha kuwa sio rahisi kuvitenga hivi viti kama wanavyosema wao, ila ni muhimu kutoiweka dini kama ndio muhimili wa siasa.
    Mfono mzuri ndio huo jamaa kasimama kwenye kadamnasi ya watu anasema assalamu aleykum, au bwana asifiwe, hapo kuna watu wa dini mbalimbali, ina maana watu wa dini nyingine wasemeje? hawataona kuwa hawahusiki.
    Hakuna ubaya kuwa mbele katika dini yako, na kila jambo unatakiwa umuweke mungu mbele, lakini watu wengine wanatafsiri kila kitu utakachofanya, hata kina nia njema wao watakitia doa, na hapo ndipo busara inapohitajika.

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU