NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, August 11, 2010

SWALI LA KIZUSHI: KIPI NI BORA, MAISHA MAFUPI KWENYE UHURU AU MAREFU UTUMWANI???

 • Kwa kisayansi aina hii ya twiga wanajulikana kama Rothschildii (Class: Mammalia, Order: Artiodactyla, Family: Giraffidae, Genus: Giraffa, Species: Camelopardalis, Sub Species: Rothschildii)
 • Porini kwenye uhuru wanaishi kati ya miaka 10 na 15 tu!
 • Utumwani kwenye mazizi ya wanyama (zoos) wanaweza kuishi hadi miaka 28
 • Swali la kizushi: Tuwaweke utumwani hawa twiga ili waishi miaka mingi (28) au tuwaache huru porini waishi maisha mafupi (miaka 10)?

  5 comments:

  1. Kwa wanyama mimi naona heri ya utumwa, kwani ni kwa afya zao, lakini kwa binadamu, mmmh, utumwa mwingine sio mchezo, utatamani ardhi ipasuke udidimie, sijui wenzangu mwasemaje

   ReplyDelete
  2. Mimi ningependa kuishi maisha mafupi kwenye uhuru. Maana kuna utumwa ambao ni hatari kwa hiyo afadhali nife mapema tu...

   ReplyDelete
  3. Mimi naona hayo ni maisha ya ubwanyenye, chakula analetewa, maji anapewa, matibabu kama akiugua, na pia hana wasiwasi wa kushambuliwa na wanyama wengine kama simba nk.
   Yaani ni sawa na maisha anayoishi rais, sijui utaita ni utumwa au... maana kila kitu anafanyiwa, mpaka kuandaliwa hotuba, kila anapotaka kwenda basi hawezi kuammua ni saa ngapi aende, mpaka walinzi wampe go ahead, hawezi hata kwenda pub kufurahia kilaji, haruhusiwi kutembea mwenyewe, mavazi ya kisela marufuku, matibabu mpaka afuatwe nyumbani, yaani kila mahali alipo lazima mtu mwingine ajue, sasa urais ni utumwa au... Na watu wanagombea mpaka kukaribia kutoana nyoyo.
   Ni mtazamo wangu tu kwa upande huu wa shilingi

   ReplyDelete
  4. Dkt. Chib;

   Mtazamo mzuri chokonozi au pengine niseme fikirishi. Niliwaona Twiga kutoka Afrika kule Honolulu kisiwani Hawaii na japo wanapata huduma ulizozitaja ni wazi kwamba wako utumwani (pengine tuite utumwa wa raha!)

   Wana kajisehemu kadogo sana ka kukaa na kotekote kumebanana. Siku yote wanashinda wamejilaza tu kwani hawana la kufanya na chakula chao mara nyingi ni cha kuletewa. Kusema kweli hawana uchangamfu kama wale wenzao niliowana kule Manyara. Inawezekana ni kwa sababu, kama ulivyosema, hawa hawana wasiwasi wa kuliwa na simba n.k. Ingewezekana tungewauliza wao wangependelea maisha ya aina gani - kule Serengeti kwenye uhuru (japo kuna mikikimikiki kibao) au zizini Honolulu (kwenye utumwa wenye raha!)

   Kuhusu mfano wako wa rais na "raha" zake hapo sina maoni. Pengine wenyewe maraisi watuambie kama uraisi ni "utumwa ama la!" Na kama ni utumwa, ni kwa nini wanakukuruka kugombea na kuhakikisha kwamba wanabakia "utumwani" kwa kutumia kila njia iwezekanayo? Ndiyo tuseme kuna utumwa mtamu na utumwa chukizi?

   ReplyDelete
  5. Prof Matondo, ukiangalia shilingi kila upande, ina uzuri wake na ubaya wake. Inategemea wewe unaangalia upande gani. Kwa hao twiga, mie naona wana shida, na hawana uhuru

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU