NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, August 19, 2010

TUSIENDESHE HUKU TUKITUMA UJUMBE KWENYE SIMU ZETU. NI HATARI !!!

 • Baadhi yetu hatuwezi kujizuia kutuma ujumbe mfupi kupitia simu zetu kwenda kwa marafiki au kuweka katika kurasa za facebook na twitter. 
 • Kama vile nilivyowahi kuonyesha hapa, wanasayansi wameshathibitisha kwamba tabia hii ni ya hatari zaidi kuliko hata kuendesha ukiwa umelewa pombe au bangi. 
 • Suala hili limezuka tena baada ya daktari mmoja wa watu maarufu aitwaye Frank Ryan kuporomoka na gari lake na kufariki kule Malibu. Malibu ni sehemu ya milima mingi na barabara nyingi ni nyembamba na zenye kona kali. 
 • Polisi wamethibitisha kwamba, daktari huyu alikuwa anatuma ujumbe katika akaunti yake ya twitter juu ya mbwa wake kabla ya gari lake kuacha barabara na kuporomoka kwenye makorongo milimani. Daktari alifariki hapo hapo lakini mbwa wake alipona. Kwa habari zaidi kuhusu habari hii bofya hapa.

TUWE WAANGALIFU !!!

2 comments:

 1. Sijui kwanini baada ya kusoma ujumbe nikajiuliza hivi ni wangapi Tanzania wenye tatizo hili.

  Nikimaanisha :
  Kwanza; wanasimu ambayo watatuma meseji
  Pili; wana gari.

  Kuna matatizo fulani huwa na wahusika wake tu. Ni kama tu ukiwa kijiji fulani cha Wapare halafu ulalamike kuhusu Pizza wakati watu ni wala kishumba.:-(

  NAWAZA tu kwa sauti!

  ReplyDelete
 2. Mtakatifu. Pengine ni wachache lakini pia hata kama angekuwa mmoja bado ni muhimu. SMS sasa ni mojawapo wa njia muhimu za mawasiliano na nadhani karibu kila simu ina uwezo wa kutuma meseji.

  Nilipokuwa Dar es salaam hivi karibuni niliwaona wengi tu wakiendesha na huku wanatuma meseji. Hata rafiki yangu aliyenipeleka uwanja wa ndege siku naondoka alikuwa anatuma meseji wakati gari liko moto.

  Mimi mwenyewe nimeshawahi kufanya hivyo wakati wa rush hour na kidogo nigongwe. Pengine hata wewe Mtakatifu umeshajaribu. Ni tabia ya hatari sana!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU