NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, August 10, 2010

UNATAKA KUISHI MIAKA 100 NA ZAIDI? SOMA UTAFITI HUU.

 • Wengi wetu tunapenda kuishi maisha marefu kwa kadri iwezekanavyo. Maendeleo ya sayansi na teknolojia na hasa maendeleo makubwa katika taaluma ya tiba na kuimarika kwa hali ya maisha kwa ujumla hasa katika nchi zilizoendelea kumeleta uwezekano wa watu kuishi miaka 100 na hata zaidi.
 • Katika utafiti mpya kabisa, wanasayansi, wanaonya kwamba watu wachache wanaoishi miaka 100 na hata zaidi  wanafanya hivyo kutokana na sababu za kibayolojia/kimaumbile. Watu hawa wana chembechembe za uhai maalumu ambazo zinawasaidia kutopatwa na magonjwa ya kawaida yanayosababisha vifo kwa wazee. 
 • Baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa chembechmbe za uhai za watu 1000 wenye umri wa miaka 100 na zaidi, wanasayansi sasa wanaweza kutabiri kwa usahihi wa asilimia 73 uwezekano wa mtu kuishi hadi kufikisha miaka 100 na zaidi. 
 • Kama una wazazi, babu na bibi, wajomba, mashangazi, na ndugu wengine wa karibu ambao waliishi hadi miaka 100 au zaidi basi kuna uwezekano mkubwa kwamba familia au ukoo wenu umeshinda bahati nasibu ya kimaumbile ya kuishi maisha marefu. 
 • Pamoja na hayo, wanasayansi wanaonya kwamba hata kwa watu ambao wamejaliwa kurithi chembechembe hizi nzuri za urithi, bado wanahitajiwa kuishi maisha yenye kuzingatia afya njema mf. kufanya mazoezi mara kwa mara, kutokunywa pombe kupindukia, kutovuta sigara na kutonenepa kupindukia. 
Angalizo letu kuhusu suala hili: 
 • Tunaungana na Marcus Aurelius (a.k.a Mwenye hekima) -  mtawala wa himaya ya Roma ya kale kutoka mwaka 161 mpaka kifo chake mwaka 180 B.K. alivyosema katika kitabu chake cha Meditations alichokiandika kati ya mwaka 170 na 180 B.K kwamba:
  “Hebu tazama kipindi kirefu kilichopita nyuma yako, na muda mrefu usio na kikomo ambao haujaja bado. Katika ombwe hili la muda kuna tofauti gani kati ya yule anayeishi siku tatu na yule anayeishi vizazi vitatu?”

Ati, kuishi miaka 100 au zaidi kutakusaidia NINI?
 • Kwa muhustasari wa maoni ya kifalsafa kuhusu suala la kifo kutoka katika blogu hii, bofya hapa.

3 comments:

 1. Miaka mia kwa mbongo, sijui atakuwaje, manake hebu angalia hali halisi ya sasa, mtu akifikia miaka 80, yupo hoi bin taaban, sasa akamilishi 20 zaidi!
  Kusihi ataishi lakini cha moto atakionyesha kwa wanaoishi naye! Kijijini wapo lakini utawaonea huruma, na inahitajika mtoto wake wa karibu awe anye lakini kama utamkabidhi `mka mwana' mmmh, atanyanyaswa

  ReplyDelete
 2. Ati, kuishi miaka 100 au zaidi kutakusaidia NINI?

  Hakuna - yote ni kujilisha upepo tu...Kumcha Mungu na kuyatenda mapenzi yake ndiyo kusudi letu sisi binadamu hapa duniani.

  ReplyDelete
 3. sidhani kama natamani kuishi miaka yooote hiyo. lazima niondoke kwenye mwili tu

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU