NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, August 26, 2010

USIKONDE. HATA "MAJUU" KUNA KUNGUNI KIBAO NG'WANAWANE !!!

Picha hii inapatikana hapa.
 • Marekani sasa inakumbwa na tatizo kubwa la kunguni na Jiji la New York ndilo linaongoza kwa kuwa na kunguni wengi huku likifuatiwa na Philadelphia, Detroit, Cincinnati, na Chicago. Kwa majiji mengine yanayoongoza katika sakata hili bofya hapa. Wataalamu wengi wanasema kwamba kunguni sasa limekuwa tatizo la kitaifa hapa Marekani na serikali kuu ya shirikisho imeshaombwa kusaidia katika baadhi ya sehemu zilizoathirika zaidi. 

3 comments:

 1. Pole sana hao ni wadudu wabaya sana, sisi huku wakati wa summer tulikuwa tunasumbuliwa sana na kupe.

  ReplyDelete
 2. Nafikiri kwa uzoefu tulio nao sisi huku Afrika, tunaweza kutoa msaada mkubwa wa mawazo, jinsi gani ya kupambana na hawo wadudu bila kutumia dawa. maji ya moto kwa mfano nk
  Wadudu kama hawo tunao karibu maisha yetu yote, sasa tutakosa kauzoefu ka kuwashauri hawa wenzetu ambao kukutana nawo hawa wadudu kidogo tu imekuwa janga.
  Tutaomba wazoefu waitwe waje huko.
  Nakumbuka kabla sijaenda JKT, niliambiwa chawa ni rafiki wa kuruta, na huruhusiwi kumuua chawa, basi kwenye bukta yako wanaweza wakajipanga kwenye mikunjo kiasi kwamba ukipata nafasi ya kuwaua unachukua jiwe halafu unaiweka bukta kwenye jiwe jingine na kuwaponda,ta, ta, ta, mapaka bukta inabadilika rangi, halafu unaenda kufua, angalau wamepungua kidogo...sasa hako kauzoefu na tukichanganya na kauzoefu kengine kanaweza kusaidia, au!

  ReplyDelete
 3. Hawa wadudu kwa mara ya kwanza nilikutananao Sweden wakati nafanya masters.:-(

  Kuna vitu unaweza usivioanishe na sehemu lakini ukweli ni kuwa vipo. Na usishangae sikumoja kukuta usiyemdhania ndiye mwenye chawa.:-(

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU