NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, August 9, 2010

UTAFITI: ETI WANAWAKE HUVUTIWA NA WANAUME WALIOVAA NGUO NYEKUNDU !!!

 • Kama wewe ni mwanaume na ulikuwa hujafikiria kununua nguo nyekundu pengine itabidi ubadili mawazo na kuzitafuta mara moja. Utafiti mpya uliochapishwa katika Jarida la Experimental Psychology: General la tarehe 2 mwezi huu unaonyesha kwamba wanawake huvutiwa sana na wanaume waliovaa nguo zenye rangi nyekundu kuliko rangi nyingine yo yote. 
 • Utafiti huu unaonyesha kwamba wanawake kutoka katika tamaduni mbalimbali (mf. Marekani, Uingereza, Ujerumani na China) huwaona wanaume wenye kuvalia nguo nyekundu kama wenye uwezekano mkubwa wa kuwa na kipato kikubwa na wenye nafasi kubwa ya kufanikiwa maishani; na hivyo kuvutiwa nao. 
 • Katika tamaduni nyingi duniani rangi nyekundu huhusishwa na watu wenye utajiri na mamlaka. Ndiyo maana dhifa na hafla mbalimbali zenye hadhi kubwa huambatana na utandikwaji wa zulia jekundu (red carpet). 
 • Pia, katika baadhi ya wanyama, rangi nyekundu ndiyo huashiria mamlaka ya kiume na wanyama dume katika jamii za wanyama hawa huwa wamepambwa kwa rangi nyekundu. Kwa hivyo inawezekana kwamba wanawake wanapoona mwanaume aliyevaa nguo za rangi nyekundu, vionjo hivi vya kibayolojia vinavyohusianishwa na rangi nyekundu "huhuishwa" katika akili zao.
 • Kwa habari zaidi kuhusu utafiti huu bofya hapa. Makala yote kuhusu utafiti huu kama ilivyochapishwa katika jarida la Experimental Psychology: General unapatika hapa (kurasa 19, pdf)
 • Wanawake (wa Kiafrika) hebu basi mtuambie: ni kweli mnavutiwa na wanaume waliovaa nguo nyekundu??? Kama ni kweli basi naona mashati mekundu yataisha madukani...

  4 comments:

  1. Ngoja nami nifikirie upya ununuzi wangu wa nguo..

   Ha ha haaaaaa.

   ReplyDelete
  2. Hivi kweli, hebu tuambieni mwapendani katika rangi, manake wengine red, mmmh, sio ushabiki , lakini imekaa kidamudamu

   ReplyDelete
  3. Kuna shati jekundu nilinunua zamani sijui liko wapi. Aisee ngoja nikalitafute.

   Ninaendelea kuusoma huu utafiti and it seems to be tight and serious research. Dunia hii kuna a lot of things that we still have to learn

   ReplyDelete
  4. mie ishakula kwangu hapo. ntaambulia patupu. unajua kwa nini? mie yanga damu.

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU