NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, August 17, 2010

WANABLOGU WENZANGU, NIMEULIZWA SWALI "GUMU": TUSAIDIANE KULIJIBU


Wanablogu msikilizeni huyu mdau. Naliweka swali lake kama lilivyo. 
**************

Bwana Matondo. Naipenda blogu yako. Ni one of the blogs ambayo imepangwa vizuri na yenye uandishi wa pekee. Pia umefanya effort kubwa kuzicollect blogs mbalimbali na kuziarrange according to topics. Hii inasaidia kwa sisi tunaopenda kuperuse.

My big problem/question is this: mbona hukuziweka adult blogs? Kuna za mapenzi na mahusiano but not zile za ngono. Why? After Ze Utamu, ina maana hakuna blogz za ngono za Kiswahili? Au wewe na bloggers wa Kiswahili mnabagua?

If this is the case, this is NOT FAIR na mko wrong kwani blogz za ngono ndiyo popular. Nenda maofisini, mashuleni, vyuoni na sehemu zingine. Probably katika kila watu 10 walioko online, 8 of them watakuwa wanaangalia ngono. Kwa hivyo acheni unafiki washikaji. Mnavunga hampendi ngono wakati ndiyo waangaliaji wakubwa. Hivyo please add adults blogz za ngono kwenye list yako ili mambo yaende vema. Nitashukuru sana na natumaini hutaignore hii concern yangu anbayo naamini ni ya wadau wengi tu.

Ni mimi mdau mkuu wa blogu yako

J. Konga (a.k.a Mzee wa Mikong'oli) 
Buguruni.

11 comments:

 1. Ni vyema ukamfahamisha kuwa kuna masharti ya kuanzisha blog. Kama blog yako umeianzisha kuandika vitu vya kawaida huwezi tena ukaingiza vitu vya kikubwa(Adult).
  Sio unafiki kama anavyodai, kwani kila kitu kina masharti yake. Huwezi footbal ukacheza kwa mkono, ni faulu, au sio. Kama nikuziweka hizo blog unaweza ukaziweka na kuainisha kuwa ni za `adult only' lakini tuelewe kuwa unapomuonyesha mtoto kuwa kitu hiki sio kwa watoto anakuwa na hamu sana ya kujua ni nini kilichomo, na matokeo yake atakichungulia, hii ipo na kwasababu wote tumepitia utoto tunaifahamu na kwa wewe mwalimu inazifahamu vyema tabia za kitoto!

  ReplyDelete
 2. Katika akili zangu nilijua kila mtu anaruhusiwa kuandika atakacho na kuweka kwenye orodha yake atakacho.

  ReplyDelete
 3. Ndugu Matondo, kwa mtizamo wangu hadhi ya blogu haifanani na mapendekezo ya mdau huyu. Namshauri mdau kujiunga na global publishers nadhani huku anaweza kutuliza kiu yake kwa kiasi fulani.

  ReplyDelete
 4. Huyu msomaji wako ni mpuuzi. Kama anataka blog za ngono ambazo mara nyingi hushambuliwa kirahisi na virusi basi aende huko huko kwenye ngono zake. Hatuwezi kuishi kwa mambo ya ngono kama udaku wa Bongo. Kama anachoataka kwenye blog hakipo aende huko kilipo. Ni haki yake kuangalia ngono. Kadhalika ni haki ya Matondo kutotangaza ngono. Dunia inakimbia na falsafa na sayansi. Wasio na muelekeo wanawazia ngono! Makaye ga mbiti!

  ReplyDelete
 5. Mdau muuliza swali. Nadhani umepata majibu ya kuridhisha kwa swali lako. Mimi napenda tu kuongezea kwamba, huu ni wakati wa Google na mtandao ni pori na unaweza kupata karibu kila kitu unachokitafuta humo. Lakini jihadhari, vingine ni vya hatari! Tuendeleze libeneke lakini kwa kuzingatia amali za jamii, heshima na nafasi zetu kama memba wa jamii ya Tanzania.

  ReplyDelete
 6. Kazi kweli kweli. Watu waache utoto? Kwanini yeye asianzishe hiyo blogu yake ya ngono. Kwani anataka kipi ya zaidi ya hivyo anavyoviona huko kwenye mablogu ya ngono?

  ReplyDelete
 7. Ni kweli kwamba tumeumbwa kutokana na ngono, lakini ngono si jambo ambalo tukilikosa basi ndo mwisho wa maisha yetu kama ambavyo tukokosa oxygen kwa sekunde kadhaa uhai wetu unapotea.

  Kama jamaa alivyosema zipo blog nyingi za ngono anataka nini toka kwa Deus Mapumba Nzuzullima? Au kwakuwa yeye ni mtaalam na mpenzi wa ngono. Ikoje hiyo?

  ReplyDelete
 8. nadhani ana point huyu jamaa, tumekulia katika jamii za kujifanya hutupendi ngono wala mapenzi wakati mawazo yetu yamejaa hizo tu! na tunahitaji shule pia, nadhani ni tatizo kubwa linalopaswa kuwekwa hadharani

  tujiulize sote changamoto zitokanazo na ngono, kwa mfano uwapo safarini, ugonjwa nk, nini kinatutokea kwenye hisia za ngono? kama hatupendi mambo hayo, mbona tuna ndoa na tunapata misukosuko kwa sababu hiyo??

  sijui lakini nadhani ana point huyu jamaa

  ReplyDelete
 9. Issue si kwamba ngono ni kitu cha hovyo. Ngono ni kitu cha binafsi sana -private. Kama wanaounga mkono ngono watwambie kama watafurahi kuangalia blog za ngono na watoto wao. Maana yake ni kwamba si kila kitu kinaweza kuwa public jamani tuache ulimbukeni na kudandia mambo. Suppose mwanao anafungua blog yako anakumbana na mambo ya kipuuzi yanayopaswa kuwa private utamfunza nini? Mbona huku ulaya hata vyombo vya habari vinajitahidi kuziepuka kama ndiko mnakoigiza? Sijui kama itaingia akilini kuwaambia BBC au CNN eti waanzishe vipindi vya ngono. Huu kwao ni udaku ambao ni saizi ya malimbukeni kama Shigongo na Mabambataa na mavuvuzela limbukeni wa vyombo uchwara vya ubomoaji maadili.

  ReplyDelete
 10. Chambilecho ChimwagaAugust 20, 2010 at 2:14 AM

  Samahani mdau - inabidi tui-edit comment yako ya jana...
  *******************
  Niliweka comments zangu mbili naona umezitoa: WHY? I am posting one of them and please don't delete them. Hakuna mtoto among us so why the fear??? Blogz zenu zinakuwa kama za watoto bwana. Don't dissapoint basi!

  If yo a looking for a swahili adultz blog just vizit **********************

  pLIZ don't delete thiz message

  ReplyDelete
 11. honger sana NN Mhango kwa mchango mzuri kwa huyo limbukeni........badala ya kuwaza mambo ya maana ye anawazia ngono......ama kweli omba umaskini wooooooooooote lakini cio umaskini wa mawazo
  ndo unajikuta unakurupuka tu kama unatoka chooni.wakat wenye akili wanadiscuss vitu vya maana mpuuzi anawaza ngono tuuuuuuuuu

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU