NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, August 30, 2010

WASUKUMA NJOONI HUKU TUJICHEKE: TUMETANIWA NA MHEHE!!!


CHEKA UNENEPE.

Msukuma mmoja alibahatika kwenda zake Uingereza, baada ya kufika alishangaa uzuri wa mji na majengo ya kushangaza.

Ili akirudi Tanzania awakonge wenzake kila alichokiona alitaka kujua kinamilikiwa na nani. Cha kwanza kuuliza kilikuwa kujua uwanja ule wa ndege unamilikiwa na nani. Alimuona Mzungu mmoja amesimama alimfuata na kumuuliza.

“Eti uwanja huu wa ndege ni wa nani?”
Speak English,” Mzungu hakumuelewa na kumuomba azungumze Kiingereza.

Jamaa baada ya kuelezwa vile aliondoka akiamini anayemiliki ule uwanja ni Speak English. Alipoondoka pale alikwenda hoteli moja kubwa na kuulizia ile ni ya nani, aliyemuuliza kwa Kiswahili hakumuelewa alimjibu “Speak English.”

Kila kona alielezwa vile, basi jamaa aliporudi Tanzani aliamini Speak English ndiye tajiri mkubwa nchini Uingereza. Kila kona aliwaeleza jinsi kila kona alipouliza watu kuhusu mmiliki wa vitu vya thamani aliambiwa Speak English.

Watu walimcheka na kumueleza Speak English siyo tajiri bali walimueleza azungumze Kiingereza kwa vile walikuwa hawamuelewi akizungumza kiswahili. Mmh, hii kali kujua lugha nako raha. 
Aliyetutania hivi anapatikana hapa.
*******************

6 comments:

 1. ha ha ha haaaa safi sana. Hakujua hata mabugando yanamilikiwa na huyo huyo Speak English. Wasukuma bwana.

  ReplyDelete
 2. ha ha ha haaaa safi sana. Hakujua hata mabugando yanamilikiwa na huyo huyo Speak English. Wasukuma bwana.

  ReplyDelete
 3. Utani bwana, sasa hebu tujiulize huyu mtu alipitaje hadi kuingia Uingereza, kwani uwanja wa ndege angeulizwa passport kwa kiingilshi au nako aliulizwa kisukuma!

  ReplyDelete
 4. Hahaaa hahaaa PROF Matondo, imekugusa sana eheee, na bahati yako sio mtani wangu mbona ungeipata....

  ReplyDelete
 5. Fadhy - inawezekana hata libugando linamilikiwa na huyo huyo Speak English.


  Emu-three - kweli. Msukuma huyu alipitapitaje uhamiaji pale Heathrow mpaka akaingia Uingereza kwa tajiri Speak English?

  Edna - hii imenifurahisha sana. Unajua utani ulikuwa sehemu muhimu ya utamaduni wetu ingawa sasa, kama vile sekta mbalimbali za utamaduni wetu, utani nao unatoweka.

  Hivi Wahehe nyie kumbe siyo watani wetu eeh! Sasa kama siyo watani wetu mbona umetutania???

  Nilikuwa nimeanza kutafuta kautani fulani kanakohusu kula kambwa na kwa vile umeanza kujitetea kwamba wewe si mtani wetu basi ngoja nikuache!

  Ngoja nami nikazane ili siku moja nitajirike kama Sir "Speak English!"

  ReplyDelete
 6. Hahaaa! Hii imenichekesha sana,hivi hii speak English ni msukuma peke yake au hata wahehe huambiwa speak English?

  Kaka huyo Edna huyo ni mtani wetu gete!gete! asikudanganye ili usimtanie,mtanie sana tu.

  Ila kusema ukweli kaka wasukuma sio siri kwa ushamba hatujambo,hii sio yakuhadithiwa niliishuhudia mwenyewe Tabora mjini,miaka ya themanini mwishoni naikumbuka vizuri sana,siku hiyo ilikuwa j'5 saa moja jioni tunatoka shule kwenye mazowezi ya umiseta,kufika kwenye msikiti wa jamatini tukakuta kuna mtu kawa kama kichaa......msukuma maskini ya mungu katoka kuuza pamba yake katapeliwa na matapeli ya mjini 800,000= miaka hiyo ilikuwa sawa na mamilioni ya sasa, eti kauziwa msikiti wa jamatini,saa hizo wenyewe wahindi wanakwenda msikitini na vicheuro vyao mkononi, anawafukuza na fimbo yake mkononi,alikuwa kama mbogo...watu walijaa wakimshangaa akidai hiyo ni nyumba yake kainunua....watu walizani ni mwendawazimu kumbe ni mzima na akili zake timamu ni mpaka polisi walipofika ndio kumtuliza na kuanza kumhoji kuliko? ndio akaanza kujieleza na kuonyesha makaratasi hewa ya kumiliki nyumba na taa zote zinazowaka,kilichoendelea sikujua tena maana ilibidi aondoke na polisi kwenda kituoni kumhoji zaidi.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU