NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, September 15, 2010

MAISHA YA KIJIJINI, AMRI ZISIZOTEKELEZEKA NA "UPOFU" WA WATUNGA SERA

 • Sijali kama eneo hili ni hifadhi inayolindwa. Sijali kama ni shamba la mtu binafsi. Sijali kama....Kama eneo hili lipo maeneo ya kijijini amri hii itavunjwa na watu watalivamia na kuanza kukata kuni.
 • Ati, kama hujawapatia nishati mbadala, na tayari walishakata karibu miti yote (mf. kule Shinyanga) unategemea watapikia nini au unataka wale vyakula vibichi? Watu wa vijijini (ambao ndiyo wengi) ni kama vile wamesahaulika, na halafu wewe mtunga sera na watekelezaji wako mnakurupuka na kwenda kubandika tangazo kama hili bila kujali na kuangalia mahitaji halisi ya watu wanaoishi pale. 
 • Swali: Amri hii ikivunjwa, tumchukulie nani hatua? Ni hao akina mama hapo juu ambao hawana njia nyingine ya kupikia vyakula vyao au huyo mkazi wa mjini ambaye ametoa hii amri?
 • Mtazamo na mantinki hii tenge ndivyo husababisha miradi mingi isiyo shirikishi katika jamii - miradi ambayo inapendekezwa na watunga sera waishio "dunia nyingine" bila hata kwenda kuangalia hasa maisha ya walengwa wa miradi hiyo yakoje na kama wakitakacho watunga sera ndicho kinachotakiwa na walengwa. Matokeo yake miradi hii haifiki popote, halafu tunaanza kupiga makelele na kulalamika kwamba walengwa wengi wa miradi hii hawajasoma, hawasaidiki wala kuendelezeka. Kumbe ukiangalia vizuri tatizo hasa ni sisi "tuliosoma" ingawa kusema kweli bado hatujaelimika!
Picha ya pili na ya tatu ni kutoka kwa Mjengwa. Ya kwanza sikumbuki niliipata wapi.

2 comments:

 1. Jambo hili la watu wengine kuwatungia waguswao kimaisha wengine ndilo lililonifanya mpaka nibishane mpaka na wale wapingao kukeketwa kwa wanawake ambao hawatoi suluhisho kwa wananchi ambao tamaduni zao zimejengeka na misingi yenye ukeketaji.

  Huwezi kumkataza mtu kitu kama huyo mtu unamuacha bila kumjengea suluhisho la ufikirialo ni kitatua tatizo kwa kuwa ila kieleweke hata kwa kuvunja sheria atakeketwa tu kisa anafikiri ni kitu kitakacho mfanya apendwe katika jamii , aheshimike kwenye jamii au tu aonekane tu kama shujaa KIBANGA ampiga MKOLONI.:-(

  Ndio,...
  hapa naunga mkono hoja aliyotoa Profesa Masangu Matondo Nzuzullima.

  ReplyDelete
 2. sio upofu bali kukosa UTASHI wa kisiasa na kimaadili katika utekelezaji!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU