NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, September 28, 2010

CHACHACHA, TAI NA SHATI LISILOCHOMEKEWA WAPI NA WAPI? MAISHA YA KUMBUKONI.

 • Kwa mliokuwepo, mnazikumbuka chachacha? Kweli jamani tumetoka mbali na picha hii inanikumbusha mambo mengi sana. Hapa ni kidato cha nne, Shule ya Sekondari ya Kahororo Bukoba kwa watani zangu wenye matatizo sana na herufi h-. Ukitaka kuona "homework" yangu ya Fizikia ya kidato cha nne gonga hapa.
 • Miaka nayo inakimbia wanguwangu na siamini kama tayari ni zaidi ya miaka 20 tangu picha hii ipigwe. Maisha!
 • Angalizo:  Methali yangu niipendayo sana niliyojifunza huko Bukoba ni hii: Ebigambo bingi bikatanga enkoko okwikukusa!!!  Methali hii imegeuka kuwa falsafa (mojawapo) ya muhimu sana katika maisha yangu.

  7 comments:

  1. Hakika ttumetoka mbali CHACHACHA mweeh! yaani umenikumbusha mbali mno lakini unajua sasa hivi hizo chachacha zinarudi tena. Ya zamani ni mali ni vitu vya zamani inasemekana kuwa ni imara zaidi.Kumbukumbu nzuri hata kama tulikuwa tunaungua motooooooo

   ReplyDelete
  2. Ohh! nimerudi tena nilisahau kitu, nahisi hii methali:- Ebigambo bingi bikatanga enkoko okwikukusa!!! ina maananisha MTAKA CHA UVUNGUNI SHARTI AINAME AU MVUMILIVU HULA MBIVU!!

   ReplyDelete
  3. wewe ngoja jua liwake saa sita mchana.

   hii methali inamaanisha 'matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno'

   ReplyDelete
  4. Kweli tupu. Kumbe mnazikumbuka chachacha. Jua likiwaka zinapata moto zinalainika na ikibidi itakulazimu uzivue. Kazi kwelikweli.

   Hiyo methali nitamwachia Kamala aitafsiri lakini nadhani Mwaipopo umekaribia zaidi. Pole Dada Yasinta.

   ReplyDelete
  5. Mcheza kwao hutunzwa, nafikiri wanaotoka huko wanaijua zidi yetu.
   Chacha na yeboyebo ni mtu nduguye, lakini zile chacha, zilikuwa zikibana vizuri mguuni, tatizo jua likiwa kali...mmmh, kazi kwelikweli!

   ReplyDelete
  6. Emu-three unanitaja mimi ama?....lol!

   Nakumbuka sana hizo zi viatu....lol!

   ReplyDelete
  7. Watani wangu "WAMA-THAI" chachacha hazipitwi na wakati!!!!

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU