NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Saturday, September 11, 2010

ETI KIINGILIO NI SH. LAKI MOJA! KWENDA KUANGALIA WASICHANA VIMBAUMBAU "WAKIREMBUA"?

Jisomee zaidi hapa
*****************
Mpambano wenyewe - Laki moja ndiyo hiyo inakwenda!!!

Warembo waliofanikiwa kuingia nafasi tano bora ikiwa ni fainali ya kumpata Vodacom Miss Tanzania 2010, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi…
 

Warembo waliofanikiwa kuingia nafasi kumi bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa…

Mrembo akianguka jukwaani wakati akipita na wenzake na vazi la ufukweni Duh aibu we acha tuuu.

Warembo wakipita jukwaani na vazi la Ufukweni….
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wakifurahia jibu la Mrembo Pendo, aliyemfagilia Rais Jakaya Kikwete wakati akijibu swali lake aliloulizwa.

**************************
 Na Hatimaye Mrembo kuliko wote Tanzania Ndiye Huyu!!!


Vodacom Miss Tanzania 2010 Geneviv Mpangala (katikati) akiwa na washindi wenzake msindi wa pili, Glory na Consolata, baada ya kutangazwa washindi katika kinyang’anyiro hicho kilichofanyika katika uku bi wa Mlimani City Mwenge Jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo

Picha zote na maelezo (mengi) ni kutoka hapa
5 comments:

 1. Na watu wanazitoa hizo lakini wakiambiwa mtoto hana kitabu na wala hana sale za shule anasema sina hela...kaazi kwelikweli..

  ReplyDelete
 2. You have a very nice blog! Good reading.
  Drunknmunky - Pikavippivinkit

  ReplyDelete
 3. Mmmmh hii ndio Tanzania yetu akitoka hapo anaenda kuchangia kitchen Party,sendoff,harusi nk.Kama ulivyoseama Yasinta mtoto akisema hana vifaa vya shule anasema hana pesa.

  ReplyDelete
 4. Ahsanteni wachangiaji mumegusa hisia zangu, kwamba starehe ni kwanza mengine baadaye...ndio maana hatuna madakitari wa kutosha, mainjinia, na w....mmmh wanasiasa tunao kibao!

  ReplyDelete
 5. Hawa mashabiki wa kuona uchi ndiyo wanaweza eti kumnyooshea kidole dr. Slaa! Kweli nyani haoni kalio lake. Huyo mkuu wa mkoa Lukuvi ni kihiyo anayedaiwa kughushi vyeti vya kitaaluma. Unategemea apate wapi taamuli ya kujua jema kitaifa zaidi ya kuishi na kufanya kazi kutokana na kulipana na fadhila kunakofanywa na rais wenu mtalii bingwa wa mieleka?
  Wenye mapenzi na Danganyika au mizengwe lieni na kujipaka majivu mkivaa magunia kuomboleza msiba mkuu wa nchi kuendeshwa na wababaishaji na majambazi. Tufanye nini? Soma kitabu changu cha SAA YA UKOMBOZI uone wanyonge tena wa kijijini wanavyoangusha utawala mfu na mchafu wa Mizengwe ukiachia mbali kushuhudia mkuu wa mkoa akinguka jukwaani.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU