NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, September 1, 2010

HILI TANGAZO NI LAZIMA LIMEANDIKWA NA MHAYA

 • Mzee wa Changamoto na Kamala msije mkanipiga mawe. Herufi [h] inawachachafya sana. Inapotakiwa mnaiondoa na isipotakiwa mnaiweka. Kwa sisi Wasukuma, tuna shida sana na herufi [r] (mf. nimeshapiga kula). Kule kijijini Mataranyirato tatizo lipo kwenye herufi [l] (mf. kura tumekura pa kurara je?). Wachaga wana shida na herufi......Picha ni kutoka Mtaa kwa Mtaa

6 comments:

 1. Ha ha haaa. Jeraha au Mtelezo wa ulimi. Mpaka na kuandika

  ReplyDelete
 2. we mwaipopo file fiatu fyako fyeupe fiko wapi?
  mambo ya kyela na tukuyu hayo

  ReplyDelete
 3. Mzee wa Kiraracha: Wananji wa Tanzania, nji hii inahitaji rais mpya. Nipeni uraisi wa nji hii muone mabadiliko...

  ReplyDelete
 4. wahaya hatutaki shida, hatulazimiki kuchagua / kulemba maneno kama wengine, wacha, si ujumbe umefika? kwa nini aweke H kuharibu nafasi yake na wino wake?

  ReplyDelete
 5. Kulingana na maoni ya Mwaipopo tunaweza kuongezea kwamba huko Kyela na Tukuyu herufi [v] inawapa shida.

  Maoni ya mdau anony - yanaonyesha kwamba kule Kiraracha (sijui ni wapi) herufi [ch] hawaiwezi.

  Kamala - Ni kweli hajaharibu nafasi na wino wake lakini sina uhakika kama ujumbe umefika sawasawa kama alivyotarajia.

  Tatizo ni kwamba [h] ndiyo mofimu ya ukinzani (negation) katika Kiswahili na unapoitoa au kuiongeza unakuwa unatangatanga katika ule mstari mwembamba wa hasi na chanya. Una uhakika hapa kwamba ujumbe umefika???

  ReplyDelete
 6. Wairaqw sisi tunashida na Z na S, mfano, badala ya Z tunatumia S, ZEZE, tunasema SESE. Neno SEMA, Mwiraqw anaweza akatamka kama ZEMA.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU