NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, September 6, 2010

MAKARATASI YOTE YA TALAKA KWA DOLA 199.99 TU !!!

  • Nililiona hili tangazo jana kando ya barabara karibu kabisa na hapa ninapoishi. Inasemekana sasa kiwango cha talaka hapa Marekani kimefikia karibu asilimia 50 - yaani karibu nusu ya ndoa zote zinazofungwa zinaishia katika talaka.
  • Tuombe "balaa" hili lisije likatukumba kwani talaka zina athari nyingi hasa kwa watoto. Nchi za Skandinavia ambazo ndizo zinaongoza kwa masuala ya usawa wa kijinsia pia ndizo zinaongoza kwa kuwa na viwango vingi vya talaka. Sina uhakika kama kuna uhusiano kati ya usawa wa kijinsia na talaka. Tuwe macho!

2 comments:

  1. labda vinaendana, ila wanaodivoce wanapata shida baada ya ku-divorce kwani hugundua kuwa nje ya ndoa kwaweza kuwa kugumu kuliko ndani mwa ndoa na watu huachana kwa kiburi mbali mbali kikiwemo cha haki sawa lakini pia inafuatana ni kitu gani kiliwasukuma kuaona kama ni cha muda au hadaa basi wakigundua vinginevyo huachana!

    ReplyDelete
  2. Matondo, hili suala la usawa kati ya mwanamke na mwanaume ndiyo chimbuko la yote haya. Hapa kwetu rais mwanamke, waziri mkuu mwanamke, ukifika maofisini na makazini mabosi wengi wanawake. Wanaume hawana sauti kabisa katika mambo mengi, unaweza hata kumpenda mwanamke lakini huna jeuri ya kumwambia hivyo hata mgengekuwa karibu namna gani ili kukwepa zali, utabakia hivyo hivyo na maumivu yako hadi yeye aanzishe,utaratibu mwingine wa maisha!

    Wazungu saa zingine wanajipendelea, utakuta mwanamke au mwanamme anatafuta separation au divorce baada ya hapo atafanya mahusiano yasiyo rasmi na wengine wengi tu,lakini mtu mweusi akifanya hivyo watasema practices of polyandry or polygamy

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU