NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, September 28, 2010

MBUNGE WANGU (MZEE WA VIJISENTI) MATATANI - MAHAKAMA YATOA AMRI AKAMATWE MARA MOJA !

 • Wakati akiwa katika kampeni za ubunge na Mwenyekiti wa chama chake, kesi ya Mheshimiwa Andrew Chenge iliendelea kuunguruma katika Mahakama ya Kinondoni bila ya yeye kuwepo wala wakili wake.
 • Kutokana na utoro huu, hakimu Fimbo aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo aliamru Mh. Chenge akamatwe mara moja 
 • “Haijalishi kuwa mshitakiwa yuko kwenye kampeni au wapi, Mahakama haitambui jambo lolote kuhusu kampeni, hivyo kwa kuwa hajahudhuria mahali hapa, inabidi akamatwe kwa kushindwa kutekeleza amri ya Mahakama,” alisema Hakimu Fimbo.
 • Ni kweli amri ya mahakama itatekelezwa na mheshimiwa huyu kukamatwa? Ni lazima pia "tujivunie" demokrasia YETU WENYEWE tunayoiendesha kwani katika nchi zingine ni nadra sana kukuta wagombea ambao wana kesi kubwa mahakamani wakiendelea kugombea nafasi kubwa za kisiasa - na wakategemewa kushinda!

12 comments:

 1. Mwana wane pole sana kama mbunge wako ni mwizi Chenge. Bongo, nawaonea huruma sana watu wanaowakilishwa na watu wenye matumbo makubwa tamaa ya fisi kama huyu wako, Lowassa, Mramba, Rostam na wahindi wengine ambao kuchaguliwa kwao hakumaanishi chochote zaidi ya ubwege wa watu wa majimbo yao.
  Angalia akina Nshomile walivyowabwaga mafisadi wao yaani Niziro Kadamage, Nimorod Mkono na Daktari Feki Dolorous Kamala. Kwa vile wachaga ni wezi hata wanyamwezi, hawawezi kuwawajibisha wezi wao tajwa hapo juu ukiachia mbali wanyantuzu wanaomuabudia Chenge wakati ni kibaka wa kawaida hata kama anaitwa msomi. Usomi wake hauna tofauti na wa Kawambwa wala wale vilaza walioghushi vyeti. Zamani niliwapenda sana watu wa Bariadi. Lakini walipogeuzwa nyumba ndogo na huyu habithi sina hamu. Nilizoea kwenda kujipumzisha kule Ngeme, Mwamapalala, Bunhnamp'hala,Zagayu hata Kashishi na Kasori. Siku hizi nikipata fursa huwa najipumzisha Lushoto au Ukerewe.

  ReplyDelete
 2. Wewe NN Mhango. Kuwa na respect na civilization kidogo kwenye blogu za wenzako. Siyo tu unakwenda unatukana watu hovyo kila mahali kama kule kwenye blog yako. What did CCM do to you such that you hate it so much? Is there anything GOOD that CCM did for our country au whatever they do ni kuiba na kupora nchi tu? Your blog is full of hatred (which is different from criticism) and it painful even to read it. Punguza hasira kijana utakuja kufa mapema!!!

  ReplyDelete
 3. Mimi nahisi Chenge anaidharau mahakama, kama alijua ana kesi tarehe ilipofika, mbona hakutokea.
  Nakubaliana na siasa za wastaarabu, maana wao wakituhumiwa kwa jambo kubwa au wakiwa na kesi ya jinai, hawashiriki katika kugombea uongozi. Lakini wapo wengi tu, akina Mramba na wengineo

  ReplyDelete
 4. Chib nakuunga mkono kwa asilimia zote.

  ReplyDelete
 5. Anonymous you are but a bugger (senge) sorry for this. Mie nilishakufa zamani. Hivyo siogopi kufa. Mbona Kikwete wenu hajaikandia CCM lakini anaanguka anguka hovyo?
  Kufa si issue wala big deal bali reality. Umeficha jina lako kwa sababu ni miongoni mwa mabwege au mafisadi niliowataja. Nitaichukia CCM hadi siku tutakapoing'oa na kuwafunga hata kuwaulia mbali mafisadi wanaoitumia kutuibia kwa kisingizio cha kututawala.

  ReplyDelete
 6. Mr. NN Mhango.

  I am the anony that you are calling a "bugger"

  You need to see a Psychatrist there in Canada as soon as possible before it is too late. It will help you.

  And for the rest of us - let us jut IGNORE this lunatic who spews poison and hatred-calling people names - every time he opens his mouth.

  ReplyDelete
 7. Pamoja na matatizo na heka heka hizi zinazomkabili naamini kwamba Mheshimiwa Chenge atashinda uchaguzi bila wasiwasi. Shida pengine itatokea kama atahukumiwa kwenda jela katika baadhi ya kesi zake zinazomkabili. Chenge anapendwa sana na wapiga kura wake - jambo ambalo kwa sisi "wasomi" na welewa wa mambo tunaweza tusilielewe - na hata kufikia kudai kwamba wapiga kura wa kijijini ni "wajinga!"

  Nilipokuwa kijijini mwezi wa sita mwaka huu nilipata muda mzuri wa kuongea na wanakijiji na nilitaka kujua yupi wangemchagua katika uchaguzi wa mwaka huu. Bila kusita na moja kwa moja walibainisha kwamba mbunge wao wa siku zote atakuwa ni Mh. Chenge. Walitaja sababu nne za msingi kwa nini Chenge anawafaa:

  (1) Chenge anayajua matatizo yao na huwa hasiti kuwasaidia wanapokuwa na shida. Yeye hana cha kusubiri wala mambo ya urasimu. Ukiwa na shida anakusaidia hapo hapo - hakuna cha njoo kesho wala nini. Wenye wagonjwa wanasaidiwa, wenye kuhitaji baisikeli wanapewa hela wakanunue, wenye kuhitaji karo za shule wananunuliwa n.k.

  (2) Chenge amesaidia sana kuzima makali ya chama cha UDP ambacho kilikuwa kimejitandaza Bariadi kabla ya ujio wake katika medani ya ubunge. Na japo wanampenda Mzee Cheyo - mwenyekiti wa taifa UDP na Mbunge wa Bariadi Mashariki - hawapendezwi na baadhi ya wagombea wa nafasi za udiwani wa chama hicho ambao walikuwa wanawahisi kuchochea fujo. Walitaja pia kwamba chama cha UDP kinahusishwa na vitisho na mambo ya kutumia ushirikina kuwatisha wagombea wa upinzani. Jambo hili linawakera wapiga kura na Chenge kwao ni mtu wa muhimu katika kupunguza makali ya UDP.

  (3) Chenge ni mtu safi na anaandamwa na watu wasiomtakia mema yeye binafsi na jimbo lake. Tena hawataki kabisa kusikia mambo ya rada na kashfa zingine. Hata ajali zinazomwandama ni njama tu za kishirikina za wabaya wake wanaotaka kumwangamiza. Lakini Chenge naye ni kiboko na walisema kwamba anaogopwa sana na hakuna mchawi anayeweza kumchezea.

  (4) Tayari ameshaanza mipango ya kujenga barabara ya lami kuunganisha makao makuu ya Mkoa mpya (Bariadi) na Lamadi kitu ambacho kitasaidia sana. Tayari kuna Wachina ambao wamepiga kambi karibu na shule ya Sekondari ya Bupandagila wakisubiri kuanza ujenzi wa barabara hiyo ya lami. Walisema kwamba kama angeingia mtu wa UDP basi barabara hii isingejengwa kwani serikali ya CCM haitaweza kujenga barabara hiyo wakati kuna mbunge wa upinzani.

  Kutokana na sababu hizi, nilitambua jambo moja: Wanakijiji hawa wanajua mahitaji yao na wanajua ni nani anayewafaa. Kwa sisi "wasomi" tulioko mijini tunaweza kupiga makelele na kuwalaumu wapiga kura wa kijijini kwamba ni "wajinga". Inabidi twende huko na kuwasikiliza ni kwa nini wanawachagua watu ambao kwetu wanaonekana wana utata. Daima kuna kitu cha kujifunza na hii ni nafasi nzuri ya kufahamu hasa aina ya demokrasia tunayoiendesha.

  Mwalimu Mhango (a.k.a Mpayukaji) - huna haja ya kunipa pole kwa sababu eti Chenge ni mbunge wangu. Pamoja na tuhuma zote zinazomkabili - na kama wapiga kura wake wanamhitaji aendelee kuwaletea maendeleo - sisi ni nani mpaka tuseme vinginevyo? Bariadi ni mji unaokua kwa kasi na maendeleo yanaonekana.

  ReplyDelete
 8. Mwalimu Matondo, ulipoleta hoja hii ya Chenge na 'ujinga' wa wanavijiji kwa mara ya kwanza nilitoa maoni yangu lakini ninafikiri kutokana na 'ujinga' wangu wa kutumia teknolojia ya kisasa huenda ikawa nilibofya pasipo. Kwa ufupi, nilikuwa nimeeleza nilivyokuwa nimekunwa na mjadala huo, na nilitaka kuchangia tu kwa kuwakumbusha wasomaji kuhusu adui wetu wakuu wanaotambuliwa rasmi la serikali ya ccm tokea uhuru ambao ni umaskini, maradhi, na ujinga. Maadui hawa wote wameendelea kutusumbua na pengine kuongezeka maradufu. Na sababu za wanavijiji kwa mzee wa Vijisenti ulizozibaini vizuri zinathibitisha jinsi adui 'ujinga' alivyojiimarisha. Kwa maoni yangu sio tu kuwa adui 'ujinga' anawakabili wakulima maskini, bali pia ametanda kwa 'wasomi' kuanzia vyuo vikuu vya Dar na Dom hadi maofisi ya kimataifa! Kwa taarifa tu, ni kwamba ameongezeka adui mwingine mkubwa - ufisadi- huyu hatambuliwi rasmi na serikali ya ccm lakini ndiye adui mama wa maadui. twafwa!!!
  Mlalahoi,
  kwa mfugamafisadi

  ReplyDelete
 9. Mwl. Masangu naheshimu sana mawazo yako. Sema tunatofautiana kwenye uoni na kina cha uoni. Sipendi mbunge anayeibia taifa ili 'kuendeleza' jimbo lake. Mwl. Nyerere angekuwa na nyongea na upogo kama huu, wewe nami tusingesoma hadi kufikia hapa tulipo. Hivyo, hoja hapa si 'maendeleo' bali namna yanavyoletwa-kwa pesa ipi na toka wapi? Ni hatari kama wote tungekuwa na wabunge kama nyemelezi kama Chenge. Tulishuhudia ujambazi huu kule Mwanga na Rombo ambapo wabunge wao walisifika sana kuleta 'maendeleo' yaliyotokana na pesa ya kuhujumu taifa. Huu ni ufisadi wa kimfumo. Kama tutapanua mawazo, tutakubaliana kuwa hii ni hongo na kudhalilishana. Na kimsingi, hili ndilo tumeshuhudia kwenye chaguzi za ndani za CCM. Kila mtu kahonga. Rais naye kila siku anaonekana akihonga kuokoa madaraka yake ambayo kimsingi ni kwa ajili ya kujinufaisha, familia, washirika, waramba viatu wake na mbweha wengine wengi waliomzunguka kwa kuangamiza nchi.

  Kwanini Chenge kama waziri na mwanasheria mkuu wa zamani awe na kiu ya maendeleo ya jimbo lake lakini si taifa lake? Hii ni sawa na mtu kukata shina akitaka kuliokoa tawi asijue mti mzima utaanguka.

  Kuhusu la Chenge kutokuwa na umangi meza, ni kweli kama utamlinganisha na wachovu wengine waliotamalaki kwenye ofisi za umma. Heri kuwa na mtu mmangimeza kama waingereza lakini akaleta maendeleo ya taifa lake na kuwa mwadilifu.

  Anachofanya Chenge na wenzake kama Lowassa, Mkono, Mramba, Dewji, Abood na mafisadi na magabacholi wengine waliojiingiza kwenye siasa ni sawa na baba kuiba pesa ya familia nzima ili kumnufaisha mtoto mmoja asijue wengi wanateseka.

  Kuhusiana na mchango wa rafiki yangu bugger au Anonymous wa kunitisha kifo na kudai kuwa ufisadi si adui anayetambulika kitaifa, kuna haja ya kufikiri tena. Maana ufisadi ndiyo mama wa maadui aliowataja.

  Jamaa huyu aliyebakwa na kukeketwa akili alinitisha kifo utadhani yeye ni Mungu. Naomba Mungu amuondoe kabla yangu. Maana mie napigania watanzania yeye anapigania mafisadi. Na inshallah kuna siku ataujua ukweli. Mtaanza kuanguka na kuumbuana hadi mmalizane kabla umma haujawamaliza. Kama wewe ni bingwa wa kuua wakosoaji anza na kina Marando, Slaa na wengine walioko mstari wa mbele kumkabili Mungu wenu na baba yenu anayewalinda.

  ReplyDelete
 10. ...tatizo si 'ujinga' wa wanavijiji bali RAMBARAMBA!

  ReplyDelete
 11. Nimefurahi jinsi ulivyoweza kuongea na wanakijiji na kuona mtazamo wao. Nyie educated mtapiga makelele na CHADEMA na harakati zenu lakini bila kuwaelewa wapiga kura wa kijijini analysis zenu za vitabuni ni useless.

  Kama villagers wanamwona Chenge kuwa ni mkombozi wao nyie mtapiga makelele ni fisadi mpaka mtachoka. We need to go to the villagers, talk to them and educate them on the issues. Otherwise, our theories and complicated academic analysis are USELESS

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU