NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, September 23, 2010

NI KWELI KWAMBA WATU WA VIJIJINI NI WAJINGA WASIOTAKA KUELEWA UKWELI?

 Picha ni kutoka kwa Mpayukaji
******************
Katika mada yangu ya Siasa za Maji Taka, Anony wa September 21, 2010 4:57 AM alitoa maoni yafuatayo:

***********************
Ni kudanganyana kwa kwenda mbele. Tatizo la wananachi hasa walioko wilayani na vijijini ni wajinga wasiotaka kuelewa ukweli. Anakuja mgombea anaahidi MAISHA BORA kwa kasi mpya na nguvu mpya! Baada ya Miaka 5 anarudi na kuwapa ahadi nyingine lukuki tena za anasa kama viwanja vya ndege vya kimataifa na hosipitali za rufaa, mishahara minono kwa wafanyakazi wote. Watu wote lukuki walioenda kumsikiliza (hawazuiwi kwenda) wanasima na kupiga makofi na kusema na kuimba nambari waniiiiiiiiiix2.

Ukiwatizama kwenye hizo picha unaona wanaishi katika maisha yaliyokata tamaa, mazingira na sura choka mbaya sasa sijui hayo ndio maisha bora walioahidiwa. Kwanini wasihoji tu hapo kuwa maisha bora yamepelekwa wapi? Watoto wachanga na wajawazito wanapoteza maisha kila siku (Takwimu zisizo sahihi ni kama 20 kwa siku!), Maajali ya kila siku yanaongezeka barabarani na lawama zinapelekwa kwa madereva, ndio madereva wanamakosa, sasa wanafanywa nini ili kuwarekebisha? Au ndio kama mwendo wa kuomba kura (kula?) wakati wa uchaguzi. Elimu i nazidi shuka chini, watoto kibao wanafeli kidato cha nne (chukulia asilimia 20, ndio wanafaulu). Kilimo kinazidi kurudi nyuma ihali wachache wanakuwa makabaila(kwa kujilimbikizia mashamba) na kudai eti kilimo kwanza? Ukienda pale Meatu au Mpanda au Lushoto ukamwuliza mkulima maana ya kilimo kwanza hajui! DUH huu ni upumbavu mkubwa sana! Samahani.
  
**********************
 • SWALI: Japo pengine kuna ukweli fulani katika maoni ya huyu anony, swali ninalotaka kuuliza hapa ni hili: Ni kweli watu wa Wilayani na vijijini ni wajinga wasiotaka kuelewa ukweli? 
 • Pengine inabidi tujiulize: Ni kwa nini walimpokea Mheshimiwa Chenge kwa mapokezi makubwa yasiyowahi kutokea katika wilaya ya Bariadi baada ya ile kashfa yake ya vijisenti? Naamini pia kwamba Mheshimiwa Chenge (ambaye ni mbunge wangu) atashinda tena kwa kishindo katika uchaguzi huu. Atashinda kwa sababu eti wapiga kura wake ambao wengi ni watu wa kijijini ni wajinga wasiotaka kuelewa mambo?
 • Tukiweza kutambua ni kwa nini hasa watu hawa wa kijijini na wilayani bado wanachagua viongozi wao wapendwa ambao katika macho yetu sisi "wenye uelewa" wana madoa ya ufisadi na kashfa zingine tutakuwa tumepiga hatua katika kuelewa aina ya demokrasia tunayoiendesha. 

4 comments:

 1. Matondo,siyo kwamba watu vijijini ni wajinga, la hasha. Shida ni umasikini ulikithiri. Wananchi hufikiria leo na siyo kesho, hivyo mtu akishapata ukika wa kuishi leo anasahau ya kesho.

  Chenge na mafisadi wenzake wenye pesa wanao uwezo wa kumaliza matatizo madogo madogo ya wananchi wao kwa malipo ya kura, mambo yote ni "KULA NA KURA",samahani kwa ndugu zangu Wakurya, Wahaya na Wasukuma, Hahahaa. Hivyo basi tatizo siyo ujinga ni ukosefu wa mwamko miongoni mwa wananchi hasa wale wa sehemu za vijijini.

  ReplyDelete
 2. Huyo Bwana "Vijisenti" ni mkombozi kwa wana Bariadi.

  Hata leo hii serikali ikiruhusu wagombea huru, atashinda na kuingia Bungeni!

  Ni aina mpya ya "warlordism)!

  ReplyDelete
 3. Mzee wa vijisenti Oyee!!! CCM Oyee!!! Hakuna wa kumshinda Chenge Bariadi ni mpaka tu atakapochoka mwenyewe. Lakini anasifika pia kwa kutologeka kwake. Wachawi wameshajaribu wakashindwa na sasa hakuna la kufanya mpaka tu atakapochoka mwenyewe.

  I like the man kwa sababu ni honest. Tuacheni utani. Hata nyie mnaopiga makelele hapa kweli mkipewa uwaziri mtaacha kuiba? Chenge kapata nafasi ya rada kachota mabilioni yake, nyie mmebakia mnapiga makelele yeye anapeta tu. Niko Mwanza and I will vote for him in this election

  ReplyDelete
 4. Nilipokuwa kijijini niliongea na wanakijiji na nilitaka kujua yupi wangemchagua katika uchaguzi huu. Bila kusita na moja kwa moja walibainisha kwamba mbunge wao wa siku zote atakuwa ni Mh. Chenge. Walitaja sababu nne za msingi kwa nini Chenge anawafaa:

  (1) Chenge anayajua matatizo yao na huwa hasiti kuwasaidia wanapokuwa na shida. Yeye hana cha kusubiri wala mambo ya urasimu. Ukiwa na shida anakusaidia hapo hapo - hakuna cha njoo kesho wala nini. Wenye wagonjwa wanasaidiwa, wenye kuhitaji baisikeli wanapewa hela wakanunue, wenye kuhitaji karo za shule wananunuliwa n.k.

  (2) Chenge amesaidia sana kuzima makali ya chama cha UDP ambacho kilikuwa kimejitandaza Bariadi kabla ya ujio wake katika medani ya ubunge. Na japo wanampenda Mzee Cheyo - mwenyekiti wa taifa UDP na Mbunge wa Bariadi Mashariki - hawapendezwi na baadhi ya wagombea wa nafasi za udiwani wa chama hicho ambao walikuwa wanawahisi kuchochea fujo. Walitaja pia kwamba chama cha UDP kinahusishwa na vitisho na mambo ya kutumia ushirikina kuwatisha wagombea wa upinzani. Jambo hili linawakera wapiga kura na Chenge kwao ni mtu wa muhimu katika kupunguza makali ya UDP.

  (3) Chenge ni mtu safi na anaandamwa na watu wasiomtakia mema yeye binafsi na jimbo lake. Tena hawataki kabisa kusikia mambo ya rada na kashfa zingine. Hata ajali zinazomwandama ni njama tu za kishirikina za wabaya wake wanaotaka kumwangamiza. Lakini Chenge naye ni kiboko na walisema kwamba anaogopwa sana na hakuna mchawi anayeweza kumchezea.

  (4) Tayari ameshaanza mipango ya kujenga barabara ya lami kuunganisha makao makuu ya Mkoa mpya (Bariadi) na Lamadi kitu ambacho kitasaidia sana. Tayari kuna Wachina ambao wamepiga kambi karibu na shule ya Sekondari ya Bupandagila wakisubiri kuanza ujenzi wa barabara hiyo ya lami. Walisema kwamba kama angeingia mtu wa UDP basi barabara hii isingejengwa kwani serikali ya CCM haitaweza kujenga barabara hiyo wakati kuna mbunge wa upinzani.

  Kutokana na sababu hizi, nilitambua jambo moja: Wanakijiji hawa wanajua mahitaji yao na wanajua ni nani anayewafaa. Kwa sisi "wasomi" tulioko mijini tunaweza kupiga makelele na kuwalaumu wapiga kura wa kijijini kwamba ni "wajinga". Inabidi twende huko na kuwasikiliza ni kwa nini wanawachagua watu ambao kwetu wanaonekana wana utata. Daima kuna kitu cha kujifunza na hii ni nafasi nzuri ya kufahamu hasa aina ya demokrasia tunayoiendesha.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU