NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, September 1, 2010

PALIPO NA HASI PIA KUNA CHANYA: KUNA LOLOTE JEMA KUTOKA AFRIKA/TANZANIA???

 • Kwa sisi tunaobeba maboksi hapa Marekani tumeshazoea. Ukiona Afrika inatajwa katika CNN au FOX News na vyombo vingine vya habari, basi ujue ni lazima kuna janga la kimaumbile limetokea au pengine ni njaa, umasikini, magonjwa, ukame, ukeketaji wa wanawake, vita na masaibu mengine. Ni nadra sana kuona jambo jema likitangazwa kuwa limetokea Afrika.
 • Katika darasa langu la Language in African Society ninalofundisha muhula huu, niliwauliza wanafunzi wa Kimarekani kuhusu taswira iwajiayo akilini mara wasikiapo bara la Afrika likitajwa. Kama nilivyotegemea wengi wao walitaja njaa, maradhi, umasikini, vita, rushwa, uchafu, magonjwa (UKIMWI na Malaria) na maisha mafupi. Ni mwanafunzi mmoja tu ambaye ameshawahi kufika Kenya na Senegal ndiye alipinga maoni haya na kutaja ukarimu, ubinadamu, furaha na kuheshimu mazingira. Wenzake walimshangaa mpaka alipoeleza kwa kina alikuwa anamaanisha nini.
 • Naamini hata ramani hii ya Tanzania ni mwendelezo wa mtazamo huu hasi kuhusu bara la Afrika na watu wake. Ati, kuna lolote jema linalotokea Afrika na Tanzania? Kama hasi na chanya hukamilishana, mbona mambo chanya hatuyaoni?
 • Mara nyingine ningewaomba waandaaji wa ramani hii wajaribu kutengeneza ramani inayoonyesha mambo chanya ya Tanzania halafu tuone ramani hiyo itaonekanaje.

4 comments:

 1. Kaka hapo umenena, ni kweli hawa watu wa mataifa ya Magharibi hawajui zuri kuhusu Africa...Mimi nafikiri Media zinachangia kwa kiasi kikubwa kuwapotosha hawa watu, kama ulivyosema ukiona habari yoyote kuhusu Africa inaongelewa CNN,BBC basi itakuwa inahusu uhasi na si uchanya.

  ReplyDelete
 2. ´´Good news is no news ``-so they say!:-(

  ReplyDelete
 3. Nimeguswa sana na hisia za wanafunzi wako. Ninaona jinsi gani vyombo vya habari vya magharibi vinavyoegemea upande mrama.

  Nina imani ukiwauliza watoto wa Afrika, wanaweza kukupa picha tofauti kabisa.

  ReplyDelete
 4. hata hapa nilikuwa na mmarekani mweusi, anashangaa kuona watu wanakula chakula kizuri na kushiba na anashangaa kuona tunaishi kwenye nyumba bora nak ufanya kilimo bora

  usiongelee ukarimu na utu

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU