NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Thursday, September 30, 2010

PROFESA AFUKUZWA KAZI KWA KUTOA KAULI YA "KUDHALILISHA" WANAWAKE WA KILATINO

Picha ni kutoka Grinning Planet
 • Profesa mmoja wa Sayansi katika Chuo Kikuu cha Florida amefukuzwa kazi baada ya kutoa kauli darasani kwamba eti wanawake wa Kilatino huvaa nguo zenye kutamanisha zaidi kuliko wanawake wa Kimarekani. 
 • Profesa huyo pia anadaiwa kuwa na tabia ya "kuwakazia macho" wanafunzi wa kike kwa jicho ambalo huwanyima raha na huko nyuma alishawahi kuonywa mara mbili kuhusu mahusiano yake yasiyorishisha na wanafunzi wa kike ikiwemo kugusa nywele zao na kumlazimisha mwanafunzi wa kike kucheza muziki darasani baada ya simu yake ya mkononi kuita/kulia. 
 • Profesa huyu amepinga kufukuzwa kwake na amekata rufaa akidai kwamba maprofesa inabidi wawe na uhuru kamili wa kujadili masuala mbalimbali darasani bila kuogopa kuchukuliwa hatua.
 • Wanafunzi hapa Marekani ni "wafalme" na kashfa ndogo tu - hata iwe ya kusingiziwa inaweza kumletea mwalimu matatizo makubwa. Hapa inabidi kuwa mwangalifu sana na hasa kwa sisi wageni (weusi) kwani tofauti za kitamaduni tu zinatosha kukuletea kasheshe mpaka ukashangaa. Inabidi "kubeba maboksi" kwa uangalifu kweli kweli!!!
 • Habari kuhusu mkasa huu zinapatikana hapa na hapa.

2 comments:

 1. Kama mambo yako tafu namna hii huko USA basi rudini home. Huku maprofesa wanaendelea kukanyaga wanafunzi bila noma yo yote - tena wale wazuri wazuri. Aisee uhondo unawapita.

  ReplyDelete
 2. ....sheria kama hizo zikianza huku ama kama zipo zikitekelezwa basi hatutakuwa na maprof ama watabaki wachache umno...

  Cha kushangaza hili halionekani saana...imajini suala la Prof Baregu serikali ilisema "ndiyo ni mwalimu mzuri ....lakini ni chadema!" Ujinga mtupu.

  wakati hayo yakiendelea vyuo vyetu vinatoa digrii za 'chupi' na mwanafunzi wa kiume anapoonekana ana mahusiano na mwanafunzi wa kike ambaye prof alikuwa anampigia chapuo...ndo hivo tena...kusapu ama kudisko :-(

  @Anony: ninao maprof marafiki zangu (walokuwa wazuri sana ktk taaluma) walokwisha kufa kwa ukimwi na kuna ambao wako kwenye madawa hivo si jambo la kushabikia! Inaonesha jinsi ulivo mvivu wa kufikiri :-(

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU