NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, September 10, 2010

UCHOMAJI WA KURANI HAPA GAINESVILLE NINAPOISHI - HALI BADO NI YA WASIWASI

 Tangazo mbele ya kanisa lake
 • Ni wasiwasi mtupu. Masaa machache yaliyopita huyu Mchungaji Mhafidhina (Terry Jones) alitangaza kwamba alikuwa ameahirisha zoezi la kuteketeza Kurani hapo Jumamosi saa 12 jioni baada ya kuhakikishiwa kwamba ule msikiti ulioleta mzozo kule New York ungehamishiwa sehemu nyingine mbali na "Ground Zero"
 Wafuasi wake huvaa hizi fulana
 • Mara moja, shekhe anayesimamia ujenzi wa msikiti huo tata kule New York amekanusha kwamba hajaongea na huyu Mchungaji mchoma Kurani. Huyu Mchoma Kurani sasa amecharuka upya na anasema kwamba kumbe amedanganywa na wajenzi wa Msikiti wa kule New York. Kwa hivyo uchomaji wa Kurani unaweza ukawa pale pale siku ya Jumamosi kama sehemu ya kuadhimisha mashambulizi ya kigaidi ya tarehe 11 Septemba, 2001. Kwa ujumla hali ni ya wasiwasi kwani hakuna ajuaye nini kitatokea. Mchoma Kurani huyu haaminiki na anabadilikabadilika kama kinyonga.
Alama hii ipo mbele ya kanisa lake
  • Jumamosi tarehe 11 Septemba pia kuna mechi kali sana ya mpira wa miguu wa Kimarekani hapa katika chuo kikuu cha Florida na inategemewa kwamba mashabiki wapatao elfu tisini (90,000) au zaidi watahudhuria. Kwa hivyo mapolisi, FBI na walinda usalama wa taasisi zinginezo wanahangaika kweli kweli.
  Meya wa hapa ni shoga wa wazi. Jones na kanisa lake walipinga sana kuchaguliwa kwake 
  • Tuombeni hili lipite salama lakini vinginevyo nadhani moto utawaka duniani kote. Kama vibonzo tu vya Mtume vilivyochapwa na gazeti moja la Denmark wakati ule vilileta kasheshe duniani kote, fikiria uchomaji wa kitabu kitakatifu cha Kurani itakuwaje.
   Kitabu alichoandika

   ****************************************
   Wasiwasi

   Picha hii iko hapa.

   Mwishowe: Ujumbe Mzuri

   4 comments:

   1. Kazi ipo!:-(

    On a light note:

    Kwa bahati mbaya dini za KIAFRIKA nyingi bado hazina vitabu na enzi za WAMISHENARI kuchapa WAAFRIKA viboko ili wageuze dini hazikudakwa kwenye LUNINGA,...
    ...ila sasa ule mbuyu niuabuduo kule Upareni na NGOMA zake vikitaka kuchomwa mtakiona cha utemakuni wote mdharauo dini na pembejeo za dini za wenzenu.:-(.

    ReplyDelete
   2. binadamu bwana, jamaa anahukumu uisilamu kwa kigezo cha ukristo wakati ukristo wenyewe unapiga marufuku biashara za kuhukumu.

    ila ni njia nzuri ya kujinyakulia umaarufu nakutikisa ulimwengu

    unadhani akichoma koran, zitaisha ulimwenguni?? si kauchizi tu kidogo au

    ReplyDelete
   3. kweli haka ni kauchizi, na jamaa anataka kupata umaarufu (nitoke vipi) kupitia zali ambalo mwisho wa siku watu watakiwinda kichwa chake.
    Kwa hili kamwe sililaumu kanisa (kwasababu siyo msimamo wake) lawama zote nazitupa kwa huyo mchungaji chizi.

    ReplyDelete

   JIANDIKISHE HAPA

   Enter your email address:

   Delivered by FeedBurner

   VITAMBULISHO VYETU