NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Sunday, September 26, 2010

UTAFITI: KAMA VILE UKIMWI NA EBOLA, KUMBE HATA MALARIA NAYO ILIANZIA AFRIKA !!!

 • Inavyoonekana bara la Afrika ndilo chanzo cha magonjwa mengi hatari ya kuambukiza. Baada ya "kuthibitishwa" na wanasayansi kwamba magonjwa kama vile Ebola na UKIMWI yalianzia Afrika, utafiti mpya uliochapishwa katika toleo la mwezi huu la jarida la Nature unaonyesha kwamba hata ugonjwa wa Malaria ulianzia katika nyani aina ya Western Gorillas wanaopatikana hasa nchini Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati na katika misitu ya Kongo. 
 • Unaweza kuusoma utafiti huu kwa kifupi hapa, au ufupisho wake katika jarida la sasa la Nature.  
 • Kwa nini Afrika ndiyo kiwe chanzo cha magonjwa yote haya? Ni bahati mbaya au? Sina nia mbaya bali najiwazia tu!

8 comments:

 1. Duh! sijawahi kudadisi jambo hili lakini nimejisomea kidogo ila siyo kwa kina. Natumaini ipo haja ya kuendelea kutafiti zaidi. Nakuunga mkono jambo hilo siyo nia mbaya bali ni kuwaza tu. nami naanza kuwaza sasa pengine ninaweza kudonoa donoa moja mbili tatu hivi za kuungia hoja.

  ReplyDelete
 2. Mmmh!

  Tukumbuke tu kuwa kuna magonjwa mengi PIA yalianzia ULAYA na ASIA pia.


  Ukisoma histori kidogo tu si utastukia kisa kikubwa cha kufariki kwa Wahindi Wekundu Marekani si ilikuwa ni magonjwa yaliyokuja na Wazungu kutoka ULAYA?

  Ukifuatilia magonjwa yaliyokuwa ya wanyama wengine na kuhamia kwa watu , fuatilia tu historia ya WATU tokea walipoanza kuishi na MIFUGO.

  ReplyDelete
 3. aliyefanya utafiti huo ni mwafrica au mudhungu?? lakini kuna mazuri mengi yaliyoanzia africa pia na mabaya ya ulaya, ila tusidanganyane ukimwi ulitengenezwa kwenye maabara fualani za marekani

  ReplyDelete
 4. magonjwa ni mpango wa mungu, hivyo kuanzia sehemu moja ya dunia ni mpango wa mungu pia. ila huko kwao yameanzia mambo ya ajabu ambayo sio mpango wa mungu.

  ReplyDelete
 5. Magonjwa yote yalianzia Afrika isipokuwa ufisadi, ukoloni, wizi na unafiki.

  ReplyDelete
 6. @Mpangala - sawa. Wakati mwingine tafiti hizi zinatatanisha. Ndiyo maana Bwaya huwa anahoji sana kama kweli kila utafiti unafaa kuitwa utafiti. Tuendelee kujifunza.

  Mtakatifu - ni kweli, lakini hata magonjwa hayo si ajabu ukasikia kwamba yalitoka sehemu zingine masikini. Inadaiwa pia kwamba watumwa walipeleka magonjwa kibao huko kwenye nchi ya wenyewe.

  Kamala - kuna wanaoamini kwamba virus vya UKIMWI havikutoka katika nyani wa mistu ya Kongo bali vilitengenezwa katika maabara ya chuo kikuu cha California, Los Angeles (ambacho kwa bahati nzuri au mbaya ndicho chuo nilichosoma). Pengine siku moja ukweli utajulikana lakini kwa sasa wanasayansi wote wanakubaliana kwamba UKIMWI chanzo chake ni Afrika!

  Mwaipopo - naelewa unazungumzia nini. Tazama post yangu ya kesho ambayo inaonyesha ueneaji wa kasi wa UKIMWI miongoni mwa mashoga hapa Marekani.

  Mwalimu Mhango - ufisadi, ukoloni, wizi na unafiki vilianzia wapi? Tuelimishe. Ina maana wanasiasa wetu wameiga tu mambo ya ufisadi kutoka kwingineko?

  Asanteni nyote. Tusongeni mbele.

  ReplyDelete
 7. Nyongeza:


  Ukisoma vitabu kadhaa hata cha Profesa Jared Dimond kiitwacho Guns, Germs and Steel: A short history of everybody for the last 13,000 years.

  Utakuta hawa hawa westerners wanadai moja ya kilichofanya watu kutoka eneo la kijiografia la Eurasia (Incl-North Africa) ni kwamba waishipo ndipo utakuta wanyama wengi ambao wako domesticated ndiko waliko tokea na katika uwezo wao wakuishi na wanyama mapema ulichangia kuambukizwa kwao magonjwa ya wanyama mapema na kusababisha wawe na immunity kwa magonjwa mengi mapema ambayo yalikuwa asili yake ni wanyama kama nguruwe, mbwa nk.

  Kwa hiyo sehemu nyingi walizokuwa wanakwenda pamoja na bunduki zao, moja ya silaha ilikuwa ni germs ambazo wao walikuwa na immunity lakini locals hudhoofishwa au hata kuuawa nazo.

  ReplyDelete
 8. Mtakatifu - Nitakitafuta hicho kitabu nikisome. Inaonekana ni kitabu kizuri. Asante!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU