NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Wednesday, September 29, 2010

UTAFITI: KATI YA MASHOGA WATANO MMOJA ANA UKIMWI !!!

Picha ni kutoka GLN.
 • Utafiti mpya unaonyesha kwamba kati ya mashoga watano hapa Marekani, mmoja tayari ameshaambukizwa UKIMWI; na wengi wao (asilimia 44)  hawajui kama tayari wameshaambukizwa. 
 • Wamarekani chini ya asilimia moja wana UKIMWI lakini mashoga wanaendelea kuambukizwa kwa kasi kubwa zaidi kuliko watu wengine. Ni kwa sababu hii serikali ya Marekani imeamua kuelekeza nguvu zake za kupambana na UKIMWI hasa kwa mashoga. Maelekezo mapya yanawataka mashoga wote kupima UKIMWI angalau mara moja kwa mwaka. 
 • Mashoga weusi ndiyo wanaongoza kwa kuambikizwa (au tuseme kuambukizana) UKIMWI (asilimia 28), wakifuatiwa na mashoga wa Kilatino (asilimia 18) na mashoga wa kizungu (asilimia 16). 
 • Mashoga weusi pia ndiyo wenye uwezekano mkubwa zaidi wa kutojua kama wameambukizwa  ama la (asilimia 60) ikilinganishwa na asilimia (46) kwa mashoga wa Kilatino na asilimia (26) kwa mashoga wa kizungu.
 • Kama utafiti huu ungefanyika Tanzania, hali ingekuwaje kwa mashoga wetu? Jamani mashoga na wapenda "tigo", kuweni macho! Kwa habari kamili kuhusu utafiti huu bofya hapa.

2 comments:

 1. Hapa ndipo unapoona `gharika' inavyotunyemelea'
  Swali ni je jamii, serikali na watu kwa ujumla wanalichukuliaje hili swala. Je swala la kusema `uhuru na matakwa ya watu' yasiingiliwe, ilihali tatizo hilo ni kama `ugonjwa wa kansa unaokula kidogokidogo na mwisho wa siku kutakuwa hakuna tiba tena!
  Haya, tuseme, halituhusu, lakini janga lake litakuwa haliangalii, waliokuwemo na wasiokuwemo!

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU