NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Tuesday, September 14, 2010

VIJANA - WAKATI WENU NDIYO HUU !!!

  • Vijana - hatimaye wakati wenu wa kuleta mabadiliko ya kweli na ya msingi katika jamii umefika. Bila kujali vyama vyenu, tunawaomba sana mkatangulize maslahi ya taifa na wale mnaowawakilisha mbele.
  • Nendeni mkawapiganie wananchi masikini na hasa wale wa vijijini (ambao ndiyo wengi) na kuhakikisha kwamba angalau nao wanaanza sasa kuonja utamu wa keki ya taifa.
  • Nendeni mkapambane na mfumo! Bila shaka mnazo mbinu mpya makini na kombozi za kuweza kuleta mabadiliko ya kweli ya kimfumo, na nashawishika kuamini kwamba hii ndiyo sababu mama iliyowafanya mgombee. Blogu hii inawatakia kila la heri!!!

2 comments:

  1. Ni kweli kabisa. Na wakipata mwanya huo wasifanye madudu vinginevo wabaya wa vijana hawatawaelewa..

    ReplyDelete
  2. Unategemea nini jipya kutoka kwa vijana kama January Makamba? Wewe nawe. Ni yale yale tu hakuna jipya. Ni kosa kuwalaumu wazee kwani there is no difference. Tatizo hapa ni mfumo na siyo uzee wala ujana. Ye yote atakayeingia bila kubadili mfumo ni yale yale....

    ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU