NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Monday, October 25, 2010

BILA YA KUWASIKILIZA WAKAZI WA VIJIJINI, NI KAZI BURE.

  • Si katika kura za maoni tu bali hata katika mipango mingi ya maendeleo. Hata kama iwe mizuri na kombozi namna gani, bila kuwashirikisha kikamilifu walengwa na hasa wakazi wa vijijini (ambao ndiyo wengi), kamwe hatutaweza kupata maendeleo ya kweli.
  • Hata vyama vya upinzani sijui vitautambua lini ukweli huu rahisi, kwamba kujiimarisha vijijini, katika kata, tarafa, wilaya na mikoa ndiyo hatua ya msingi kabisa kwani huko hasa ndiko ziliko nguvu za chama wanachotaka kukiondoa madarakani. Baada ya uchaguzi kupita vyama hivi vitakaa kimya na kusubiri uchaguzi ujao. Hapo tena vitakurupuka na kuzinduka kutoka usingizini huku vikitegemea tu bahati, bashasha na uchapakazi wa mtu mmoja.
  • Umefika wakati sasa vyama hivi viache mtindo huu wa bahati nasibu na badala yake vianzishe mikakati kamambe ya kujiimarisha kuanzia chini kwenda juu. Vikifanya hivi utashangaa, baada ya miaka miache tu si ajabu vikafanikiwa kuupasua mwamba ambao kwa bahati nzuri (ama mbaya) tayari umeshaanza kupata nyufa!

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU