NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, October 15, 2010

FIKRA YA IJUMAA: ATEMAYE MAKOHOZI HUPUNGUZA UGONJWA

  • Kama sikosei nilikutana na msemo huu katika riwaya ya Euphrase Kezilahabi ya Gamba la Nyoka (au Kichwamaji); na sijui kama ni msemo wa Kikerewe ama la.
  • Japo ni msemo wa kawaida tu lakini umebeba falsafa nzito. Naamini kwamba jamii yetu inasumbuliwa na kifua na iko hoi ikikohoa. Na wakati huu wa uchaguzi jamii hii ina nafasi nzuri ya kumeza ama kutema makohozi yake ili kupunguza ugonjwa unaoisumbua. 
  • Je, jamii itameza ama kutema makohozi yaliyokakawana kooni mwake ili hatimaye iweze kupumua vizuri? Jamii yenyewe inajua makohozi yake ni yapi (mapya au ya zamani?); na kwamba yanatakiwa kutemwa? Wikiendi njema wadau!

No comments:

Post a Comment

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU