NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, October 22, 2010

FIKRA YA IJUMAA: HEBU TUTAFAKARI JIBU LA HUYU MWANAFUNZI "JINIAZI"

 • Ati, kama wewe ungekuwa ndiye mwalimu ungemfanya nini mwanafunzi huyu? Ungemtandika viboko na kumtoa mkuku kutoka darasani kama mwalimu wangu mmojawapo wa hesabu alivyokuwa akifanya?
  • Jibu hili linaibua pia suala jingine gumu la kifalsafa: Jibu sahihi (au UKWELI) hasa ni nini? Tunajuaje kwamba hili ndilo jibu sahihi? Je, kuna jibu sahihi moja tu kwa kila swali?
  • Elimu - hasa hii ya darasani - imefinyangwa katika namna ambayo majibu mbadala hayaruhusiwi na kusema kweli hakuna nafasi ya mawazo "yanayotangatanga" kama ya huyu mwanafunzi mkorofi. Ndiyo maana "majiniazi" wengi kama Albert Einstein walikuwa na matatizo na elimu ya darasani hasa katika hatua za mwanzo mwanzo. Walimu kazi mnayo!

  4 comments:

  1. Mwalimu hapa umenikua kweli, mimi namsifu sana huyu mtoto ingawaje kwenye mtihani atakuwa kapa `zero' lakini katika upeo wa kufikiri ana 85% lakini `nani atamkubalia' wakati mitihani imelenga ktoa majibu ya aina moja tu!
   Huyu kijana huenda katika kichwa chake alitafakari sana, inawezekanaje mtu kushika chupa tano mkononi, au sita...na huenda zimejaa kitu...akaona `its impossible' kwahiyo wakati anatafuta `maelezo ya zida' ambayo kwenye mtihani hakuna nafasi anaikuta `time is over' umefeli mtihani....
   Mimi naamini sio kweli wanaofeli mtihani hawana akili, wanayo, ila huenda wanachofikia wao hatukuweza kukipa nafasi...
   Ni hayo mwalimu!

   ReplyDelete
  2. kiukweli hakuna jibu sahihi! kwani laweza kuwa 'debatable'

   ReplyDelete
  3. surely the teacher has a drinking problem. kinywa hunena yaliyopo moyoni. kwa nini mwalimu hakutumia maembe, peremende, apples mpaka akatumia chupa? na kwa kawaida chupa ziwekewazo vinywaji visivyolevya huwa si nyingi. wengi hawawezi kwa mfano kunywa soda chupa mbili, au juice chupa tano.

   ReplyDelete

  JIANDIKISHE HAPA

  Enter your email address:

  Delivered by FeedBurner

  VITAMBULISHO VYETU