NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, October 1, 2010

FIKRA YA IJUMAA: UBINADAMU, MADARAKA NA JAMII

*****
 • Ati, kuwa binadamu ni nini - hata kama una madaraka makubwa kuliko wote katika jamii? Nimeziona hizi picha za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nikavutiwa nazo kwani sijaona picha za aina hii zinazomhusisha mkuu wa nchi; na kwa hili naungana na Mzee wa Mtwara Kumekucha. Pia tazama hapa.
 • Hebu jaribu kuweka itikadi zako za kisiasa pembeni halafu uzitazame picha hizi vizuri halafu niambie kama unaweza kuuona ubinadamu wa binadamu - japo kwa mbali!
   • Angalizo: Mimi si mwanachama wa chama cho chote cha siasa lakini falsafa yangu kuhusu maisha ya binadamu hapa duniani iko wazi kupitia hii blogu. Wikiendi njema wadau!
   *******
   imagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.comimagebam.com
   *******

   9 comments:

   1. ......anayedhani ubinadamu uko ktk picha ni mjinga na nadhani anahitaji ushauri nasaha!

    Hicho kinachoonekana kwenye picha hizo wala si ubinadamu bali usanii kwa kibinadamu.

    ...labda ni kwa mara ya kwanza miye kuona upungufu uliokuwepo katika kufikiri kwa baadhi ya viongozi wetu. Mara ya kwanza baada ya mkuu wa kaya kuupata ukubwa alionekana akiwa kariakoo akimpa ajuza noti ya sh 10,000! sina tatizo na hilo lakini kwa fkra pevu tunahitaji sera za kuwawawezesha wazee, watoto na wasiojiweza kujikwamua bila kuombaomba.

    kitendo cha kutoa hand-outs kama pipi, hela kwa watoto/wazee/wasojiweza inaonesha kiasi gani mkuu wa nchi asivokuwa na washauri wazuri wa kuweka sera vema :-(

    ReplyDelete
   2. Chacha! UMESEMA!!!! Umesema kweli kabisa!!!! Halafuuu...why now!!!????

    ReplyDelete
   3. Kama ulivyosema Matondo wewe siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa, hata mimi ndivyo nilivyo. Lakini, napenda kusema haya kufuatia posti yako hii.

    Picha hizi ni za kinafiki kwangu mimi ni sawa tu na comedy. Huu uigizaji unaendana kinyume na matendo yake kwa wanyonge hawa. Najua dhamira yake inamtafuna kwa kuwahadaa wanyonge kwa vijizawadi,mfano suala rais kumnunulia mlemavu baisikeli siyo kwamba yeye anahuruma. Huu ni wajibu kwa serikali yake, na siyo favour hata kidogo.

    Kitendo cha raisi kuwapiga debe viongozi ambao walilazimika kustaafu madaraka yao kufuatia tuhuma za ufujaji wa fedha za walipa kodi ni ishara tosha kuwa raisi si mtu wa watu.

    ReplyDelete
   4. Nyie watu wa Chadema mnachekesha sana. Yaani hata kuwasaidia hawa wasiojiweza hapo kwa papo napo ni vibaya? Mnataka rais wetu afanye nini sasa ndipo mridhike? Yaani mnabore sana.

    Mnafikiri hata huyo padri wenu mzinzi akiingia madarakani na huyo standard 7 associate wake atafanya nini kama siyo usanii tu?

    Hizi picha zinaonyesha jinsi binadamu tunavyopaswa kusaidiana - in a good samaritan spirit. Sasa kosa la rais hapa liko wapi? kila kitu ni ufisadi ufisadi ufisadi ufisadi. Ufisadi ni tatizo la system nzima na siyo tatizo la mtu mmoja na hata padri akija hataliweza. Please give due when due. Criticisms all the time inawaharibia sana. Picha hizi zinagusa sana and I commend the prez. for being a human being on this one.

    ReplyDelete
   5. Suala la kusaidia wanyonge ni haki na wajibu wa serikali. Wala hatuhitaji kusubiri hadi wakati wa kuomba kura. Uzuri hizi picha najua chanzo chake, na pia najua zimepigwa na nani na kwa lengo gani!

    ReplyDelete
   6. Mwalimu Matondo, kwanza ninapenda kukupongeza sana kwa safu yako ya 'fikira ya Ijumaa'. Imekuwa ikinivutia na kila ijumaa ninasubiri kuichungulia. Nami nianze kwa kutoa angalizo kuwa sio mwanachama wa chama cho chote cha siasa, ila ni mshabiki wa harakati zo zote zile za kuwaletea wananchi maisha bora. Bahati nzuri, Mwalimu umeishi hapa Marekani kwa muda wa kutosha na utakuwa unajua sana kitu kinaitwa gimmicks (ujanjaujanja) hususan katika matangazo ya biashara - 'buy one get two free, tena absolutely free!'. Mkuu wa Kaya wetu ni bingwa sana wa gimmicks za kisiasa na ninaweza kumpa shahada kwa hilo. Hizi ni photo-ops tu za kuwarubuni watu(kwanza umesikia anawaambia wananchi huko vijijini kuwa "bila safari za nje tungekufa njaa" !!!!- Nipashe limeripoti). Kama ni ubinadamu kwenye phot-op basi JK ana ubinadamu usio kifani. Lakini katika safari hizo hizo: anamaliza kumpigia magoti 'mlalahoi' (ubinadamu), anapanda jukwaani kumnadi mgombea ambaye yeye mwenyewe amempeleka mahakamani kwa tuhuma za ufisadi (kesi badi hajaamuliwa na mahakama za serikali yake). Ufisadi ambao umesababisha 'mlalahoi' huyo azidi kuwa hoi (unyama). Ukisikia watu wanamwita msanii wa kisiasa usibishe!! Amekubuhu.
    bwenge

    ReplyDelete
   7. @Anony wa October 1, 2010 1:44 PM - Suala hapa nadhani si chadema wala ccm ama tlp. Suala hapa ni sera za kuwafanya watoto/wazee/wasojiweza kutoombaomba ili kutimiza haki za msingi za binadamu ili waishi kwa hadhi,utu na heshima (dignity).

    Ninapata shida sana kuona dhana ya Personal (kama ilivo corporate) social responsibility inavotumiwa vibaya na hasa wakati wa uchaguzi. I hope you get the point. Hakuna anayekataa kusaidia watu lakini utasaidia wangapi?

    kama kiongozi unatakiwa kuwa na sera inayojumuisha na siyo kufanya kitu kwa ajili ya kufurahisha watu kwa kipindi fulani ama kundi fulani...PM alilia mchozi mjengoni kutetea kuwaua wanaokutikana na hatia ya kuwaua albino LAKINI alikuwepo wakati wanampitisha anayetuhumiwa kufanya biashara ya viungo vya albino kugombea ubunge katika mojawapo ya mkoa hapa nchini.

    Kwa hiyo utaona kuwa kusema/kutoa kitu/kulia hadharani haioneshi udhati wa mtu kuwa na imani na hicho anachokililia/utoaji lakini imani hiyo itadhihirika tu pale itakapowekwa katika matendo..KUWA NA SERA inayoelekeza serikali kufanya abc kuhusu jambo fulani!!

    ReplyDelete
   8. HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKEOctober 3, 2010 at 6:25 PM

    Mtu inabidi uwe katili sana kuweza kumwangalia kilema machoni namna hii eti tu kwa ajili ya kujifanya. Huu ni ubinadamu na raisi wetu anastahili pongezi kwa hili.

    Kuhusu kuwa na mikakati imara ya kuwasaidia watu kama hawa amejaribu sana na baadhi ya matokeo yake yanaonekana. Tatizo ni kwamba mfumo wote umeoza na kuufumua wote mfumo ambao ulianzia kwenye utumwa enzi nzile mpaka wakati huu si kazi rahisi na ni kazi ya pole pole. Kazi ni ngumu zaidi ukiwa umezungukwa na watu wasioamini katika kile unachojaribu kutenda. Hata Nyerere kazi hii ilimshinda.

    This guy, with all his deficiencies I believe that he is probably the best president ambaye amekuwa karibu na watu as shown here.

    HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE!!!

    ReplyDelete

   JIANDIKISHE HAPA

   Enter your email address:

   Delivered by FeedBurner

   VITAMBULISHO VYETU