NG'WANAKANUNDO - MANJU MASHUHURI WA KISUKUMA KUTOKA MWANZA

Friday, October 29, 2010

FIKRA YA IJUMAA: UJUMBE WANGU KWA WANYANYUAJI NA WANYANYULIWA MIKONO


 KWENU MLIONYANYULIWA MIKONO (I)
 • Kwenu mliokubali mikono yenu ikanyanyuliwa na wanyanyua mikono. Ipi ni sababu hasa iliyowafanya mkubali mikono yenu inyanyuliwe? Lengo, wajibu na jukumu lenu hasa ni nini? Je ahadi mlizozitoa ni za kweli? Mtazikumbuka na kuzitekeleza?
imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.comImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image upload
 *************......*************

KWENU MLIONYANYULIWA MIKONO (II)
 • Zipo tetesi kwamba wengi wenu mmezikimbia taaluma zenu na kuhakikisha kwamba mikono yenu inanyanyuliwa kwa sababu ya marupurupu na posho hizi nono kupindukia. Kama lengo lenu la msingi ni hizi posho na marupurupu haya ya kilafi; na madaraka mengine mtakayoyapata, basi historia itawahukumu kwa kuwasaliti watu wenu waliowatuma na kuwabariki katika safari yenu ya kunyanyuliwa mikono na hatimaye kwenda "tafrijani" Chimwaga.
imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com

*************......*************

KWENU MLIONYANYULIWA MIKONO (III): WAKUMBUKENI NA HAWA
 • Hawa chini nao ni Watanzania kama nyinyi. Hawa ndiyo waajiri wenu (japo pengine hawajui). Hawa ndiyo wanaolipia hayo magari yenu ya fahari na hizo posho na marupurupu manono. Nashawishika kuamini kwamba wengi wenu lengo lenu kuu ni kuleta mabadiliko ya kweli na kuhakikisha kwamba hali za maisha za watu waliowatuma yanaboreka. Wekeni maslahi ya waajiri wenu hawa mbele, wateteeni kwa moyo na nguvu zenu zote ili baada ya miaka mitano ijayo mkaweze tena kusimama kifua mbele na "kujimwambafai" kwa maendeleo mliyowaletea.
imagebam.com imagebam.com
imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com
*************......************* 

KWENU WANYANYUA MIKONO (I)
 • Mliponyanyua mikono ya wanyanyuliwa mikono wenu na kuwaomba wananchi wawachague ilikuwa ni ishara kwamba mnawaamini wanyanyuliwa mikono wenu. Ndiyo maana minong'ono ya kutoridhika ilisikika mliponyanyua mikono ambayo wanajamii wengine walidhani ni michafu na kamwe isingestahili kunyanyuliwa nanyi. Kama tetesi hizi ni za kweli, basi tambueni kwamba kwa kufanya hivyo mmechafua pia mikono yenu na kujitia unajisi; na kwa kuwa hawa ndio mtakaowapa madaraka makubwa, wakiboronga (na pengine walishawahi kuboronga) hamtakwepa lawama za kuboronga kwao. Kuweni wakali na hakikisheni kwamba wanyanyuliwa mikono wenu wanatenda na kutekeleza yale mliyowatuma wakayatende na kuyatekeleza yaani kuinua hali ya maisha ya Watanzania wote (kama kweli hili ndilo lengo lenu). Ukuaji wa matabaka kati ya masikini (ambao ndiyo wengi) na matajiri wachache inabidi udhibitiwe. Mustakabali wa taifa zima - la wakati huu na  wakati ujao - unategemea maamuzi na uongozi wenu. Nendeni mkazitimize na kuzitekeleza ahadi mlizozitoa (kama zinatekelezeka!). 
ImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image upload
*************......*************

KWENU WANYANYUA MIKONO (II)
 • Ninategemea kwamba Ubinadamu, unyenyekevu, upendo na umakinifu mliouonyesha wakati wa kampeni na kwingineko utaendelea kujionyesha na kujidhihirisha kupitia mikakati imara itakayowaletea wananchi maendeleo ya kudumu. Kifanyeni kipindi cha miaka mitano ijayo kuwa cha vuguvugu kali la kuleta maendeleo ya kweli na ambayo hayajawahi kuonekana tangu nchi yetu ijipatie uhuru. Hatima ya Tanzania inategemea uongozi wenu. Historia ipo inawakodolea macho ninyi na vizazi vyenu!
ImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image uploadImageBam image upload
*************......*************

KWENU WANYANYUA MIKONO (III)
 • Bila kujali ni mnyanyua mikono yupi ataingia Ikulu, naomba na kutumaini kwamba miaka mitano ijayo itakuwa ya furaha, amani na matumaini kama inavyoonekana kudokezwa na taswira hapa chini. Hebu furaha, amani na matumaini yakawafikie walio wengi na hasa Watanzania wa kawaida. 
imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com imagebam.com
*************......*************
 • Japo mimi sitaweza kupiga kura, nawatakieni Watanzania wenzangu wote uchaguzi wa amani na utulivu. Mungu na Atupatie kiongozi mwenye uoni, kiongozi mwenye uchungu na nchi hii pamoja na maendeleo ya watu wake, kiongozi anayeumia na kukosa usingizi anapoona wananchi wake wakiishi katika umasikini wa kutisha, kiongozi ambaye atatuongoza kuelekea katika "nchi ya ahadi" bila kutetereka wala kumakinikia maslahi ya watu wachache tu katika jamii, kiongozi ambaye ataendelea kulinda na kudumisha mshikamano na amani  tuliyonayo. Mungu Ibariki Tanzania!
*************.....*************

5 comments:

 1. Huu uchambuzi umenigusa sana

  ReplyDelete
 2. Kila mtu atatoa isabu yake, siku hiyo inakuja.
  Ninaendelea kutafakari "fikra ya ijumaa" hii.
  Asante!

  ReplyDelete
 3. Hii si FIKRA YA IJUMAA, ni FIKRA YA MIAKA MITANO IJAYO.
  Nami ntaitunza ili siku ya siku ya siku tukumbushane kuhusu "hisabu" hii

  ReplyDelete
 4. Aiiiii. Fikra nzuri na komavu. You said it all. Ngoja tuone hawa waliovolunteer to have their hands raised watafanya nini. Inavyoonekana kila kitu kinakwenda kwa amani katika uchaguzi huu na hili ni jambo la kujivunia. Mungu Bless Tanzania

  ReplyDelete
 5. Go Kikwete Go! Good luck Mr President. Acha waseme lakini kama picha hizi zinavyoonesha, wewe ni mpenda watu na usiye na tatizo na mtu. Tena umejitahidi sana kufanya kampeni, na matokeo yameonyesha.

  Kuna kasoro ndogondogo tu ndani ya CCM na mkizishughulikia basi CCM kitabakia kuwa imara kama zamani. Kila la heri na endelea kulinda heshima na amani ya nchi yetu. Achana na hawa wahuni akina Slaa ambao lengo lao ni kutuharibia amani ya nchi yetu.

  ReplyDelete

JIANDIKISHE HAPA

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

VITAMBULISHO VYETU